• HABARI MPYA

    Sunday, December 31, 2017

    TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA LIMONGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mtangazaji wa Kituo cha Radio Uhuru, Limonga Justin Limonga kilichotokea leo Desemba 31, 2017 kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar Es Salaam.
    Kutokana na msiba huo, Rais wa TFF, Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Radio, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) pamoja na wanafamilia wote wa mpira wa miguu na wasikilizaji wote wa Radio Uhuru.
    Rais Karia amesema anatambua mchango wa Limonga na Radio Uhuru katika kupasha habari za michezo kupitia Radio hiyo.
    Pumzika kwa amani Limonga Justin Limonga. Amefariki dunia leo katika hospitali ya TMJ, Mikocheni mjini Dar Es Salaam

    Hivyo, ameguswa na kuona kuwa tasnia ya michezo na habari imepoteza hazina nyingine, lakini ametoa wito kwa wadau, familia ya Limonga, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwao.
    Limonga alihudhuria Mkutano wa Rais wa TFF, Karia na na Wahariri wa Habari za Michezo kwenye Hoteli ya SeaScape, Dar es Salaam Januari 27, mwaka huu. Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Limonga. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA LIMONGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top