• HABARI MPYA

    Saturday, December 23, 2017

    OMOG ATUPIWA VIRAGO SIMBA SC BAADA YA KUVULIWA UBINGWA ASFC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imemfukuza kocha wake, Mcameroon Joseph Marius Omog kufuatia timu kuvuliwa ubingwa wa michuano ya Azam Sports Federation (ASFC) katika hatua ya 64 Bora baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 na timu ya Green Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Taarifa ya Simba jioni hii imesema; “Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili. Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba,”.
    Joseph Omog (kushoto) amefukuzwa Simba SC baada ya kipigo cha jana dhidi ya Green Warriors 

    Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji wa klabu, Hajji Sunday Manara imesema kwamba lwa wakati huu timu itakuwa chini ya kocha Msaidizi, Mrundi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho kabla ya mapumzika Jumatatu ajili ya sikukuu ya Krisimasi.
    Taarifa ya Manara imesema timu itarudi kambini Jumanne kabla ya safari ya kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Ndanda FC mwishoni mwa mwezi.
    Aidha, taarifa hiyo imesema kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji wanawaomba radhi wanachama na mashabiki kwa matokeo ya jana. “Sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu,”imesema taarifa. 
    Omog anafukuzwa saa chache baada ya mmiliki mtarajiwa wa Simba SC, Mohammed ‘Mo’ Dewji kumtaka aachie ngazi. 
    Mo Dewji anayasema hayo kiasi cha wiki tatu tangu ashinde zabuni ya uwekezaji kwenye klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam kufuatia kutangazwa kwenye Mkutano Mkuu maalum wa Desemba 3, ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
    “Kwa kuwa bado sina mamlaka ya maamuzi kwenye klabu ya Simba, kama mwanachama na mshabiki wa Simba, namuomba OMOG kwa heshima na taadhima ajiuzulu,”amesema Mo Dewji kupitia ukurasa wake wa Twitter jioni ya leo.
    Ikumbukwe Mo pekee aliweka dau la Sh Bilioni 20 kuomba asilimia 50 ya hisa, baada ya klabu kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa Sh. Bilioni 20 miezi miwili iliyopita, ingawa baadaye Serikali ikaagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja.
    Lakini kumekuwa na tetesi za Omog kuondolewa kwa miezi miwili sasa na hata wakati Masudi Juma anawasili miezi miwili iliyopita ilielezwa anakuja kuwa Kocha Mkuu. 
    Mcameroon huyo aliyeirejesha Simba kwenye michuano ya Afrika 2018 baada ya miaka mitatu kufuatia kuipaa Kombe la ASFC Mei mwaka huu ikiifunga Mbao FC 2-1 kwenye fainali Dodoma, alijiunga na klabu hiyo Julai mwaka 2016, baada ya awali kufundisha klabu ya Azam FC na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2014.
    Omog anaondoka Simba SC baada ya mechi 79, akiipa taji moja la ASFC Mei mwaka huu na hajafungwa mechi hata moja dhidi ya mahasimu, Yanga.
    Katika mechi zake 79 tangu aanze kazi Msimbazi Julai mwaka jana, Omog ameshinda 53, kafungwa 10 na kutoa sare 16 na kati ya hizo amekutana na Yanga mara tano, mara tatu katika Ligi Kuu akishinda 2-1 Februari 26 mwaka jana (2016), sare mbili 1-1 zotd Oktoba 1, 2016 na Oktoba 28, mwaka huu (2017).
    Mechi nyingine zote alishinda kwa matuta; kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 Januari 10, 2017 na nyingine ya Ngao ya Jamii kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 Agosti 23, mwaka huu.
    Joseph Omog (kushoto) katika mchezo wa jana unaomfukuzisha kazi. Masudi Juma (katikati) anakuwa kaimu Kocha Mkuu

    REKODI YA JOSEPH OMOG SIMBA SC
    P W D L
    79 53 16 10
    1. Simba SC 6-0 Polisi Morogoro (Kirafiki Morogoro).
    2. Simba SC 2-0 Moro Kids (Kirafiki Morogoro). 
    3. Simba 5-0 Burkina Fasso (Kirafiki Morogoro).
    4. Simba SC 0-1 KMC (Kirafiki Morogoro).
    5. Simba SC 4-0 AFC Leopards (Kirafiki Simba Day)
    6. Simba SC 1-1 URA (Kirafiki Taifa)
    7. Simba 3-1 Ndanda (Ligi Kuu Taifa)
    8. Simba 0-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu Taifa)
    9. Simba 2-0 Polisi Dodoma (KIrafiki Dodoma)
    10. Simba 2-1 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Uhuru)
    11. Simba 2-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Uhuru)
    12. Simba  1-0 Azam (Ligi Kuu Taifa)
    13. Simba 4-0 Maji Maji (Ligi Kuu Taifa)
    14. Yanga 1-1 Simba (Ligi Kuu Taifa)
    15. Simba 2-0 Mbeya City (Ligi Kuu Sokoine) 
    16. Simba 2-0 Kagera Sugar (Ligi Kuu Uhuru)
    17. Simba 1-0 Mbao (Ligi Kuu Uhuru)
    18. Simba 3-0 Toto Africans (Ligi Kuu Uhuru)
    19. Simba 3-0 Mwadui (Ligi Kuu Kambarage) 
    20. Simba 1-0 Stand United (Ligi Kuu Kambarage) 
    21. Simba SC 0-1 African Lyon (Ligi Kuu Uhuru)
    22. Simba SC 1-2 Prisons (Ligi Kuu Sokoine)
    23. Simba SC 2-0 Polisi Moro (Kirafiki, Jamhuri)
    24. Simba 1-2 Mtibwa Sugar (Kirafiki Chamazi)
    25. Simba 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara)
    26. Simba 1-0 JKT Ruvu (Ligi Kuu Uhuru)
    27. Simba 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Uhuru)
    28. Simba 2-1 Taifa Jang’ombe (Kombe la Mapinduzi)
    29. Simba 1-0 KVZ (Kombe la Mapinduzi)
    30. Simba 0-0 URA (Kombe la Mapinduzi)
    31. Simba 2-0 Jang’ombe Boys (Kombe la Mapinduzi)
    32. Simba 0-0 Yanga (Penalti 4-2 Nusu Fainali Mapinduzi)
    33. Simba 0-1 Azam FC (Fainali Kombe la Mapinduzi)
    34. Simba 0-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Jamhuri, Moro)
    35. Simba 2-0 Polisi Dar (Kombe la TFF Uhuru)
    36. Simba 0-1 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    37. Simba 3-0 Maji Maji FC (Ligi Kuu Songea)
    38. Simba SC 3-0 Prisons (Ligi Kuu Taifa)
    39. Simba SC 1-0 African Lyon (Kombe la TFF Taifa)
    40. Simba SC 2-1 Yanga (Ligi Kuu Taifa)
    41. Simba SC 2-2 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa)
    42. Simba SC 3-0 Polisi Dodoma (Kirafiki Jamhuri, Dodoma)
    43. Simba 1-0 Madini FC (Kombe la TFF Sheikh A. Abeid, Arusha)
    44. Simba 1-0 Mererani Stars (Kirafiki CCM Mererani, Arusha)
    45. Simba SC 1-2 Kagera Sugar (Ligi Kuu Bukoba)
    46. Simba 7-0 Geita Gold Sports (Kirafiki, Geita)
    47. Simba 3-2 Mbao FC (Ligi Kuu Kirumba)
    48. Simba 0-0 Toto Africans (Ligi Kuu Kirumba)
    49. Simba 2-0 Rhino Rangers (Kirafiki Tabora)
    50. Simba 1-0 Azam FC (Nusu Fainali Kombe la TFF)
    51. Simba 2-1 African Lyon (Ligi Kuu Taifa)
    52. Simba 2-1 Stand United (Ligi Kuu Taifa)
    53. Simba 2-1 Mwadui FC (Ligi Kuu Taifa)
    54. Simba 2-1 Mbao FC (Fainali Kombe la TFF, Dodoma)
    55. Simba 0-0 (Pen 4-5) Nakuru All Stars (SportPesa Super Cup)
    56. Simba 0-1 Orlando Pirates (Kirafiki Afrika Kusini)
    57. Simba 1-1 Bidvest Wits (Kirafiki Afrika Kusini)
    58. Simba 1-0 Rayon Sport (Kirafiki Simba Day Taifa)
    59. Simba 1-0 Mtibwa Sugar (Kirafiki Taifa)
    60. Simba 0-0 Mlandege FC  (Kirafiki Amaan, Zbar)
    61. Simba 0-0 Yanga (Penalti 5-4)
    62. Simba 7 – 0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu Uhuru)
    63. Simba 0 – 0 Azam FC (Ligi Kuum Chamazi)
    64. Simba 3 – 0 Mwadui (Ligi Kuu Uhuru)
    65. Simba 2 – 2 Mbao FC (Ligi Kuu Mwan`a)
    66. Simba 0-0 Milambo (Kirafiki A. Mwinyi, Tabora)
    67. Simba 2-1 Stand United (Ligi Kuu Shinyanga)
    68. Simba 1-0 Dodoma FC (Kirafiki Jamhuri, Dodoma)
    69. Simba 1 – 1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Uhuru)
    70. Simba 4 – 0 Njombe Mji (Ligi Kuu Uhuru)
    71. Simba 1-1 Yanga (Ligi Kuu Uhuru)
    72. Simba 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Sokoine)
    73. Simba 0-0 Nyundo FC (Kirafiki Mpanda)
    74. Simba 3-1 Kangesa FC (Kirafiki Mandela, Sumbawanga)
    75. Simba 1-0 Tanzania Prisons (Ligi Kuu Sokoine)
    76. Simba 1-1 Lipuli FC (Ligi Kuu Uhuru)
    77. Simba 3-1 KMC (Kirafiki Chamazi, alikuwa likizo Cameroon)
    78. Simba 4-0 African Lyon (Kirafiki Chamazi, alikuwa likizo Cameroon)
    79. Simba 1-1 (Penalti 3-4) Green Warriors (Kombe la TFF Chamazi)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OMOG ATUPIWA VIRAGO SIMBA SC BAADA YA KUVULIWA UBINGWA ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top