• HABARI MPYA

    Sunday, December 31, 2017

    AZAM FC WAANZA KUTETEA KOMBE LA MAPINDUZI LEO

    Na Salum Vuai, ZANZIBAR
    MABINGWA watetezi Kombe la Mapinduzi, Azam FC wanaanza kutetea taji la oleo kwa kumenyana na Mwenge kuanzia Saa 10:30 jioni Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Azam FC inayofundishwa na kocha Mromania, Aristica Cioaba iliingia Zanzibar jana, siku moja tu baada ya ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Na baada ya mchezo kati ya Azam na Mwenge, Saa 2:15 usiku kutakuwa na mechi nyingine kati ya Jamhuri na URA ya Uganda hapo hapo Amaan.
    Azam ipo Kundi A pamoja na Simba, URA, Jamhuri na Mwenge, wakati Kundi B lina timu za Yanga SC, Singida United, Zimamoto, Mlandege, JKU na Taifa ya Jan’gombe.

    Kocha Mromania wa Azam FC, Aristica Cioaba anaanza kutetea Kombe la Mapinduzi leo kwa kumenyana na Mwenge  

    Azam watarudi tena uwanjani Januari 3, 2018 kumenyana na Jamhuri SC Saa 10:30, baadaye URA Januari 5, 2018 Saa 10:30, kabla ya kukutana na Simba Januari 6 Saa 2:15 usiku kukamilisha mechi  zake za Kundi A.
    Washindi wa pili msimu uliopita, Simba wataanza na Mwenge Saa 10:30 jioni wakati Saa 2:15 usiku Yanga watapepetana na Mlandege, mechi ambazo zitatanguliwa na mchezo kati ya Singida United na Zimamoto.
    Simba watarudi uwanjani Januari 4 kumenyana na Jamhuri Saa 2:15 usiku, kabla ya kukutana na Azam Januari 6 na kuhitimisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na URA Januari 8, 2018 Saa 10:30 jioni.
    Yanga wao watarudi uwanjani  Januari 4 Saa 10:30 jioni kumenyana na JKU, kabla ya kupepetana na Taifa ya Jan’gombe  Saa 2:15 usiku Januari 5, Zimamoto Saa 2:15 usiku Januari 7 na kukamilisha mechi zake za Kundi B Januari 8 kwa kumenyana na Singida United.
    Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Januari 8, wakati Januari 9 itakuwa mapumziko na Nusu Fainali zitafuatia Januari 10, kabla ya kilele mashindano kwa mchezo mtamu wa fainali Januari 13, ambao utahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo, Dk. Ali Mohammed Shein.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WAANZA KUTETEA KOMBE LA MAPINDUZI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top