• HABARI MPYA

    Wednesday, December 20, 2017

    MECHI YA AJABALO NA TANZANIA PRISONS ‘YAKWAMA’ KWA SABABU YA LESENI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MCHEZO wa Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya wenyeji, Abajalo FC na Tanzania Prisons umeshindwa kufanyika leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Timu zote mbili zimefika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kukaguliwa tayari kuanza, mchezo lakini wachezaji saba wa Abajalo wakazuiwa kucheza kwa sababu hawakuwa na leseni za TFF
    Mwenyekiti wa Abajalo, Edgar Chibura alisema kwamba wachezaji waliozuiwa wote ni halali na ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo.
    Chibura amesema ilishindikana kupata leseni kwa ajili ya wachezaji hao kwa sababu mfumo wa usajili wa njia ya mtandao wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), maarufu kama TMS ulikorofisha.
    “Na tangu jana sisi tulikuwa ofisi za TFF ili tuidhinishiwe wachezaji wetu na kupewa leseni, lakini TFF wamekuwa wakituzungusha tu hadi kufika hapa,”alisema.
    Inafahamika Desemba 15, mwaka huu mfumo wa usajili kwa njia ya TMS ulifeli hali iliyosababisha klabu kushindwa kukamilisha usajili kwa wakati kupitia mfumo huo.
    TFF iliagiza klabu ziwasilishe moja kwa moja usajili wake makao makuu ya shirikisho, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. 
    Lakini jana TFF ikasema kwamba TMS imefunguliwa tena baada ya marekebisho ya hitilafu zilizojitokeza kufuatia shirikisho hilo kuwasiliana na waendeshaji wa mfumo huo  walioko Tunis, Tunisia na klabu zitaendelea kusajili hadi Desemba 23 dirisha litakapofungwa tena.
    Kikosi cha Abajalo kichotarajiwa kuanza leo kilikuwa; Aaron Kalambo, Sharifu Mkangala, Laurian Mpalile, Jumanne Elfadhil, Nurdin Chona, Dotto Ramadhani, Adam Chimbongwe, Julius Kwanga, Salum Bosco, Mohammed Rashid na Eliuter Mpepo.  
    Prisons; Athumani Nyamaka, Bakari Mahadhi, Lawrence Mugia, Waziri Jitukali, Ally Abdallah, Majjid Shaaban, Kelvin Julius, Mohammed Maruzuku, Amir Ally, Ally Athumani na Hilal Bingwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MECHI YA AJABALO NA TANZANIA PRISONS ‘YAKWAMA’ KWA SABABU YA LESENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top