• HABARI MPYA

    Friday, December 15, 2017

    TAMBWE TAYARI KUANZA KAZI, KAMUSOO AANZA KUJIFUA, NGOMA NA YONDAN…

    Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
    UONGOZI wa Yanga umesema mshambuliaji wake, Mrundi Amissi Tambwe sasa yuko tayari kwa asilimia 100 kuanza kucheza baada ya kuwa nje tangu mwanzo wa msimu.
    Tambwe hajacheza mechi hata moja msimu huu, baada ya kuumia Agosti mwaka huu katika kambi ya kisiwani Pemba.
    Na akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Yanga, Dissmas Ten amesema kwamba Tambwe na kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko wote wameanza mazoezi leo.
    Lakini Ten amesema kwamba Kamusoko ameanza taratibu, wakati Tambwe sasa yuko fiti na anajifu kikamilifu tayari kuanza kucheza kwa asilimia 100.
    Mrundi Amissi Tambwe sasa yuko tayari kwa asilimia 100 kuanza kucheza Yanga

    Kuhusu beki Kelvin Yondani aliyeumia kwenye kikosi cha Tanzania Bara kilichokuwa kwenye michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya, Ten amesema kwamba atarejea uwanjani Desemba 28 na kuanza mazoezi mepesi.
    Na kuhusu mshambuliaji Donald Ngoma, Ten amesema hali yake bado haijaimarika na ataendelea kuwa nje hadi mwishoni mwa mwezi huu.
    Kuhusu usajili unaotarajiwa kufungwa leo saa sita usiku, Ten amesema katika Dirisha dogo hakuna haja ya kuongeza wachezaji wengi, kwani Yanga tayari imesajili wachezaji wawili kulingana na matakwa ya benchi la ufundi na iwapo kutakuwa na mabadiliko mengine watatangaza leo baade.
    Wakati huo huo; Mchezo wa kirafiki baina ya Yanga na timu ya Polisi Tanzania uliopangwa kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, sasa utapigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
    Ten amesema kuwa, mechi hiyo imesongezwa mbele kutokana na kuwa uwanja wa Taifa kuwa nyasi zimepunguzwa sana nakuwa chini lakini pia Uwanja wa Uhuru Jumamosi unashughuli nyingine hivyo wameamua kusongeza mbele.
    Amesema, pia wanaangalia endapo timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes ikifanikiwa kutinga hatua ya fainali kwenye michuano ya Cecafa nchini Kenya, huwenda Watanzania wengi watahitaji kuangalia mechi hiyo kupitia kwenye luninga, hivyo wanaweza kusogeza mbele muda wa mechi hata ikawa saa moja usiku.
    “Tutatoa taarifa rasmi baadae baada ya kupata matokea ya Zanzibar Heroes na kujua kama wanacheza fainali au la, na hata hivyo mechi hiyo sasa itapigwa kwenye uwanja wa Uhuru Jumapili,” amesema Ten.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAMBWE TAYARI KUANZA KAZI, KAMUSOO AANZA KUJIFUA, NGOMA NA YONDAN… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top