• HABARI MPYA

    Wednesday, December 27, 2017

    RAIS KARIA AFUTA MASHINDANO YA NG’OMBE NA MBUZI ZA WABUNGE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amefuta mashindano yoyote ya soka yaliyo nje ya mfumo wa shirikisho hilo isipokuwa tu kwa kibali maalum.
    Karia ameyasema hayo leo katika Mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya Habari nchini uliofanyika kwenye hoteli ya Sea Scape, Kunduchi mjini Dar es Salaam leo.
    Karia amesema kwamba mashindano ya soka yasiyo rasmi kama ambayo huandaliwa na wanasiasa majimboni na hata na baadhi ya taasisi na wadau, yamekuwa yakipewa umuhimu mkubwa kuliko mashindano rasmi ya TFF zikiwemo ligi.
    Rais Wallace Karia (kulia) akibadilishana mkataba na Ofisa wa Ofisa wa Marcon

    Karia amesema wakati umefika sasa Wabunge na wanasiasa kwa ujumla watoe fedha kuzidhamini timu za majimboni mwao badala ya kuanzisha mashindano ya ng’ombe na mbuzi.
    Mapema kabla ya kuanza kutoa hotuba yake hiyo, Rais Karia alisaini mkataba wa udhamini wa jezi na kampuni ya Macron.  
    Mkataba huo utakaohusisha timu zote za taifa zikiwemo za vijana na wakubwa kwa wanawake na wanaume utakuwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 800.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAIS KARIA AFUTA MASHINDANO YA NG’OMBE NA MBUZI ZA WABUNGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top