• HABARI MPYA

  Tuesday, December 19, 2017

  SANCHEZ AKATAA MSHAHARA MNONO CHINA ACHEZE MAN CITY

  MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez ameripotiwa kukataa ofay a mshahara mkubwa China huku akijiandaa na maisha mpya baada ya mkataba wake Arsenal kumalizika mwishoni mwa msimu. 
  Sanchez amebakiza miezi michache tu katika mkataba wake Emirates, ambao unamalizika mwaka 2018, na ameonyesha dalili chache za kutaka kubaki Arsenal na inaelezwa anaweza kuhamia kwa vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City.
  The Sun limeripoti kwamba Sanchez amekataa mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki kutoka klabu ya Ligi Kuu ya China, Hebei China Fortune, inayofundishwa na kocha wa zamani wa Manchester City, Manuel Pellegrini.

  Alexis Sanchez amekataa ofa ya mshahara mkubwa China wakati anataka kuondoka Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Uhamisho huo utamfanya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Chile apate hadi Pauni Milioni 21 kwa mwaka baada ya kodi – pamoja na hayo anataka kubaki kucheza kwenye ushindani wa kiwango cha juu.
  Pamoja na kwamba amepewa ofa nzuri China kuliko ambayo atapewa Man City, lakini Sanchez atakuwa tayari kupokea mshahara mdogo acheze kwenye ushndnai zaidi.
  Ikumbukwe alikaribia kuhamia Etihad kwa dau la Pauni Milioni 60, lakini Arsenal ilighairi kumuuza baada ya kumkosa Thomas Lemar kutoka Monaco.
  Sanchez anataka kwenda kuungana na kocha Pep Guardiola, waliyefanya naye kazi Barcelona awali. Lakini msimu huu ameshindwa kurudia makali yake ya misimu iliyotangulia, hadi sasa akiwa amefunga mabao matano tu katika mechi 17.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SANCHEZ AKATAA MSHAHARA MNONO CHINA ACHEZE MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top