• HABARI MPYA

  Monday, December 18, 2017

  CAF YAWAPAMBANISHA SALAH, MANE NA AUBAMEYANG

  NYOTA wa Liverpool ya England, Mmisri Mohamed Salah na Msenegali Sadio Mane watachuana kwa pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund ya Ujerumani kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mwaka 2017.
  Watatu hao wametajwa na beki wa zamani wa kimataifa wa Ghana, Sammy Kuffour katika hafla iliyofanyika mjini Accra, Ghana leo. Sherehe ya tuzo za wanamichezo bora Afrika zitafanyika Alhamisi ya Januari 4, mwaka 2018 mjini Accra.
  Tuzo ya Mwansoka Bora wa kike wa Mwaka inawaniwa na Asisat Oshoala wa Nigeria na Dalian Quanjian, Chrestina Kgatlana wa Afrika Kusini na UWC Ladies na Gabrielle Aboudi Onguene wa Cameroon na CSKA Moscow.
  Sherehe hizo zimehudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad, Makamu wa kwanza, Kwesi Nyantakyi, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Amaju Pinnick na Waziri wa Vijana na Michezo wa Ghana, Isaac Asiamah aliyekuwa mgeni wa heshima.
  Tuzo ya Mwanasoka Bora chipukizi wa Afrika inawaniwa na Krepin Diatta wa Senegal na Sarpsborg, Patson Daka wa Zambia na Liefering na Salam Giddou wa Mali na Guidars, wakati Gernot Rohr wa Nigeria, Hector Cuper wa Misri na L'Hussein Amoutta wa Wydad Casablanca wanawania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka Afrika.
  Al Ahly ya Misri, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Wydad Casablanca zinawania tuzo za Klabu Bora, wakati Cameroon, Misri na Nigeria zinawania tuzo ya timu bora ya taifa ya mwaka na timu za vijana chini ya umri wa miaka (U-20) za Ghana na Nigeria zitachuana na timu ya wakubwa ya Afrika Kusini kuwania tuzo ya Timu Bora ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAWAPAMBANISHA SALAH, MANE NA AUBAMEYANG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top