• HABARI MPYA

  Monday, December 18, 2017

  RUVU SHOOTING YASAJILI WATANO WAPYA DIRISHA DOGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Ruvu Shooting SC ya Pwani imeimarisha kikosi chake kwa ajili ya hatua iliyobaki ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kusajili wachezaji watano wapya kwenye dirisha dogo.
  Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam kwamba wameamua kusajili wachezaji hao watano ambao wote vijana ili kukiongezea nguvu kikosi katika duru ya lala salama ya Ligi Kuu.
  Bwire amewataja wachezaji hao wapya waliosaini mikataba ya kuitumikia Ruvu Shooting ni beki Rajab Zahir Mohamed, viungo Hamisi Saleh Maulid, Adam Ibrahim Abdallah na  washambuliaji Gideon Brown Benson na Alinanuswe Martin Mwaisemba.
  Rajab Zahir anahamishia shughuli zake za kisoka Mlandizi mkoani Pwani yalipo maskani ya Ruvu Shooting

  “Wachezaji hao tayari wako kambini wakiendelea na mazoezi isipokuwa Zahir pekee ambaye ataripoti kambini muda wowote kuanzia sasa,”amesema Bwire.
  Baada ya Ligi Kuu kusimama kwa wiki tatu kupisha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, Ruvu Shooting itashuka dimbani Desemba 31 kumenyana na wenyeji, Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YASAJILI WATANO WAPYA DIRISHA DOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top