• HABARI MPYA

  Monday, December 18, 2017

  GWIJI WA BRAZIL, KAKA ATANGAZA RASMI KUSTAAFU SOKA

  Gwiji wa Brazil, Kaka amestaafu rasmi kucheza soka PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  TUZO NA MATAJI ALIYOSHINDA KAKA

  Kombe la Dunia - 2002
  Serie A  - 2003/04
  Super cup ya Italia- 2004/05
  Kombe la Mabara - 05 & 09 
  Ligi ya Mabingwa - 2006/07
  Super cup ya UEFA - 2007/08
  Ballon d'Or ya FIFA- 2007
  Mchezaji Biora Ulaya wa UEFA- 2007
  Kombe la Hispania - 2010/11
  La Liga - 2011/12 
   
  Mfungaji Bora Ligi ya Mabingwa 2006/2007
  Mwanasoka Bora wa Mwaka Italia 2004 & 2007
  MWANASOKA nyota wa Brazil, Ricardo Izecson dos Santos Leite 'Kaka; ametangaza rasmi kustaafu.
  Kaka mwenye umri wa miaka 35 sasa, msimu uliopita alichezea Orlando City ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) na alisema atastaafu mwishoni mwa msimu.
  Mbrazil huyo alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Colombus Crew mwezi Oktoba - mchezo ambao timu yake ilifungwa 1-0.
  Tangu hapo haikuwekwa wazi kama Kaka atarudi kucheza mechi moja ya kuaga na timu yake ya taifa, Brazil, au atastaafu moja kwa moja mchezo alioupenda maishani mwake.
  Lakini jana ameposti kwenye mtandao wa kijamii kuweka wazi hilo.
  Aliposti picha yake isiyo ya rangi akiwa amevaa fulana yake maarufu 'Mimi ni wa Yesu' aliyoionyesha kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool, Kaka ametoa taarifa juu ya mustakabali wake.
  'Baba, Ilikuwa zaidi ya nilivyofikiria. Nakushukuru! Sasa niko tayari kwa safari nyingine. Katika jina la Yesu. Amin,"ameandika Kaka. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GWIJI WA BRAZIL, KAKA ATANGAZA RASMI KUSTAAFU SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top