• HABARI MPYA

  Monday, October 23, 2017

  NI SUPERSPORT NA TP MAZEMBE FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU ya SuperSport United usiku wa jana imefanikiwa kwenda fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Club Africain kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali uliofanyika Uwanja wa Olimpiki mjini Rades.
  SuperSport wanakwenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Lucas Moripe mjini Johannesburg, Afrika Kusini Oktoba 1, mwaka huu na sasa watamenyana na mabingwa watetezi, TP Mazembe mwezi ujao, walioitoa FUS Rabat.
  Katika mchezo wa jana, Bradley Grobler alifunga mabao mawili dakika za 16 na 64 na lingine likifungwa na Jeremy Brockie dakika ya 52 wakati bao la wenyeji lilifungwa na Saber Khalifa dakika ya 56 kwa penalti.
  Kikosi cha Club Africain: A.Dkhili; Fakherddine, Opoku/Ifa dk64, Belkhiter, Abdi, I.Dkhili, Ayadi/Darragi dk56, Khalil, Khalifa, Chenihi na Rusike/Aounallah dk78.
  SuperSport United: Williams; Nhlapo, Gould, Daniels, Modiba - Furman, Letsholonyane, Mokoena – Phala/Wome dk80, Grobler/Lakay dk68 na Brockie/Mashamaite dk60.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI SUPERSPORT NA TP MAZEMBE FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top