• HABARI MPYA

    Friday, October 27, 2017

    AZAM FC YAPAA KILELENI LIGI, YAIPIGA 1-0 MBEYA CITY

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    AZAM FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Bao hilo lilitokana na makosa ya kipa Mmalawi wa Mbeya City, Owen Chaima aliyetema mpira wa kona ya Enock Atta Agyei dakika ya 59 ukamgonga mshambuliaji wa Azam FC, Mbaraka Yusuph na kuingia ndani.
    Beki Hassan Mwasapili akajaribu kuokolea ndani mpira huo kwa kuupiga kuurudisha mchezoni, lakini refa Ole Yangalai Shakalai hakudanganyika na akawapa haki yao Azam FC.
    Mbaraka Yusuph (kushoto) ameifungia bao pekee la ushindi Azam FC leo dhidi ya Mbeya City
    Kwa ushindi huo, Azam FC inapanda kileleni mwa Ligi Kuu japo kwa muda tu ikifikisha pointi 16, baada ya kucheza mechi nane – ikizizidi kwa pointi moja moja, Simba, Yanga na Mtibwa Sugar zinazofungana katika nafasi ya pili sasa, ingawa zote zina mchezo mmoja mkononi.  
    Simba na Yanga zitamenyana zenyewe kwa zenyewe kesho Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati, Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Singida United inayoshika nafasi ya tano kwa pointi zake 12. 
    Kikosi cha Azam FC kilikuwa: Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Bryson Raphael, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Iddi Kipagwile dk68, Mbaraka Yusuph/Frank Domayo dk83, Enock Atta Agyei na Yahya Zayed/Yahya Mohammed dk73.
    Mbeya City: Owen Chaima, Erick Kyaruzi, Hassan Mwasapili, Ally Lundega, Sankan Mkandawile, Babu Ally, Mrisho Ngassa/Iddi Suleiman dk70, Mohammed Samatta, Frenk Ikobelo/Omary Ramadhani dk70, Mohammed Mkopi/Anthony Mwingira dk86 na Eliudi Ambokile.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAPAA KILELENI LIGI, YAIPIGA 1-0 MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top