• HABARI MPYA

    Tuesday, October 24, 2017

    NGOMA, TAMBWE, KAMUSOKO KUINGIA KAMBINI LEO YANGA

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    KIUNGO Thabani Kamusoko na washambuliaji, Mzimbabwe mwenzake, Donald Ngoma na Mrundi Amissi Tambwe wanatarajiwa kuingia kambini leo usiku kuungana na wachezaji wenzao wa Yanga, kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba.
    Nyasi bandia za Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam zinatarajiwa kutimbika kwa mchezo wa watani wa jadi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi kuanzia Saa 10:00 jioni.
    Na wakati kikosi cha Yanga kikiwa njiani kurejea Dar es Salaam kutoka Shinyanga ambako Jumapili walishinda 4-0 katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Stand United, Kamusoko, Ngoma na Tambwe waliokuwa majeruhi wanatarajiwa kuungana na wenzao leo.
    Thabani Kamusoko (kulia) akimiliki mpira pembeni ya kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima katika mchezo uliopita wa watani hao 
    Watatu hao hawakusafiri na timu wiki iliyopita kwa mechi za Kanda ya Ziwa kutokana na kuwa majeruhi, lakini akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Msemaji wa Yanga, Dissmas Ten amesema kwamba wachezaji hao wataungana na wenzao leo.
    “Ngoma, Kamusoko na Tambwe tayari wote wako fiti na wamekuwa wakifanya mazoezi kwa wiki sasa. Matarajio ni watajiunga na timu leo kwa mazoezi ya siku tatu zilizobaki kabla ya mechi na Simba,”amesema Ten.
    Pamoja na kuwakosa wachezaji wake hao nyota watatu kwa muda mrefu, lakini imemudu kwenda sawa na mahasimu wao, Simba katika mbio za ubingwa.
    Simba, Yanga pamoja na Mtibwa Sugar zote zinalingana kwa pointi hivi sasa, kila moja ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi saba na mshindi wa Jumamosi atatanua kwapa kileleni, wakati sare inaweza kuwashusha wote, iwapo Wakata Miwa wa Manungu watashinda dhidi ya Singida United Jumapili.    
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGOMA, TAMBWE, KAMUSOKO KUINGIA KAMBINI LEO YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top