• HABARI MPYA

    Friday, October 27, 2017

    SPURS KUMKOSA KANE MECHI NA MAN UNITED KESHO

    Nyota wa Tottenham, Harry Kane atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Manchester United kesho PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    MATOKEO YA MECHI ZA SPURS BILA KANE MSIMU ULIOPITA

    Middlesbrough 1-2 Tottenham
    Tottenham 2-0 Manchester City
    West Brom 1-1 Tottenham
    Bournemouth 0-0 Tottenham 
    Tottenham 1-1 Leicester
    Tottenham 2-1 Southampton
    Burnley 0-2 Tottenham
    Swansea 1-3 Tottenham
    TIMU ya Tottenham imepata pigo kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United wikiendi hii kufuatia kuumia kwa Harry Kane ambaye anatakiwa kuwa nje kwa maumivu ya nyama za paja.
    Spurs imetoa habari hizo asubuhi ya leo wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho mwisho kuelekea mchezo huo na United wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi.
    Wamesema kwamba baada ya kufanyiwa vipimo mapema wiki hii, imegundulika ana maumivu ya nyama za paja la mguu wa kushoto. 
    Kane aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumapili iliyipita dhidi ya Liverpool. "Kwa kesho, hatuwezi kufanya kosa kumchezesha,"alisema kocha Mauricio Pochettino kuhusu Kane.
    "Ni maumivu madogo, madogo sana, lakini hatuwezi kufanya kosa. Tutaona baada ya Jumatano Jumatano dhidi ya Real Madrid. Kesho [Jumamosi] haiwezekani. 
    "Ndiyo [ni pigo], wakati wote unataka wachezaji wote wawepo. Ni tatizo. Kucheza zaidi au kucheza kidogo, tunataka wawepo wacheze. Wakati wote tunaamini kwenye umoja, kikosi. Wakati wa msimu, matatizo yanatokea na lazima uwaamini wachezaji wote, kikosi chote,".
    Lakini msimu uliopita, ikiwa bila Kane, Spurs ilicheza mechi saba bila kupoteza, tano ikishinda. Kane amefunga mabao 13 katika mechi 12 za Spurs msimu huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPURS KUMKOSA KANE MECHI NA MAN UNITED KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top