• HABARI MPYA

  Monday, October 23, 2017

  AL AHLY YAUA 6-2 NA KWENDA FAINALI LIGI YA MABINGWA KIBABE

  TIMU ya Al Ahly jana imekuwa klabu ya kwanza kihistoria kufunga mabao sita katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa 6-2 dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia 6-2 mjini Alexandria, Misri.
  Mabingwa wa rekodi mara nane wanakwenda fainali kwa ushindi wa jumla wa 7-4  baada ya kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita, na sasa watamenyana na Wydad Casablanca ya Morocco iwikiendi ijayo, mchezo wa kwanza ukichezwa Misri.
  Iliwachukua dakika mbili Ahly kupata bao la kwanza lililofungwa na Mtunisia, Ali Maaloul aliyemtungua kipa mzoefu Ayman Mathlouthi.
  Mmorocco Walid Azaro akaifungia mabao mawili Ahly na kuifanya timu hiyo iongoze kwa 3-0 hadi mapumziko, kabla ya kukamilisha hat-trick yake dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili.
  Rami Bedoui akawarudishia bao moja mabingwa hao mara moja wa Afrika, kabla ya Ahly kupata mabao mawili zaidi kutoka kwa Hamdi Nagguez aliyejifunga na Rami Rabia na Iheb Msakni akawafungia bao la pili Etoile dakika moja kabla ya filimbi ya mwisho.
  Achraf Bencharki alifunga mabao mawili Wydad ikiifunga USM Alger ya Algeria mabao 3-1 mjini Casablanca Jumamosi baada ya sare ya bila kufungana mwezi uliopita.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY YAUA 6-2 NA KWENDA FAINALI LIGI YA MABINGWA KIBABE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top