• HABARI MPYA

    Wednesday, October 25, 2017

    TIMU 91 KUSHIRIKI AZAM SPORTS FEDERETION CUP, MICHUANO KUANZA NOVEMBA 7

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    MICHUANO ya Kombe la Shirikisho la Azam yaani Azam Sports Federation Cup (ASFC), imezinduliwa rasmi leo Jumatano Oktoba 25, 2017 kwa droo maalumu kwa timu zitakazofungua dimba kwa mzunguko wa awali.
    Droo hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko Karume, Ilala jijini Dar es Salaam ambako Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi amesema: “Michuano ya msimu huu itaanzia hatua ya awali kabla ya kuja kwa raundi ya kwanza.”
    Amesema kwa ujumla tu, michuano hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam, itashirikisha timu 91 msimu huu kwa mchanganuo wa timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL); 24 za Ligi Daraja la Pili (SDL) na 27 za Ligi ya Mabingwa wa Mkoa (RCL).
    Kwa kuanzia hatua ya awali, kundi la timu 27 la RCL timu sita zitakazocheza mechi tatu baada ya wachezaji watatu wa zamani wa timu ya taifa Abeid Mziba ‘Tekelo’, Boniface Pawasa na Salum Sued ‘Kusi’ kuchagua vitufe sita ili kupata timu hizo.
    Timu zilizopatikana katika droo hiyo hatua ya awali Buselesele ya Geita itayocheza na Green FC ya Songwe; Kisarawe United ya Pwani itacheza na Silabu ya Mtwara ilihali Usamala ya Simiyu itacheza na Sahale All Stars ya Tanga kati ya Oktoba 31; Novemba mosi au mbili.
    Raundi ya Kwanza ya ASFC itaanza Novemba 7, 8 au 9 ambako timu zilizochaguliwa kwenye droo hiyo ni kama ifuatavyo:
    Mashujaa ya Kigoma itacheza na Mshindi kati ya Buselesele ya Geita na Green FC ya Songwe; wakati mechi nyingine zitakuwa Msange ya Tabora itacheza na Milambo pia ya Tabora ilihali Bulyanhulu ya Shinyanga itacheza na Area C ya Dodoma.
    Kwa mujibu wa droo, Mji Mkuu FC ya Dodoma imeangukia kwa Nyundo ya Kigoma wakati Baruti FC ya Mara itacheza na Ambassodor ya Kahama, Shinyanga huku Eleven Stars ya Kagera ikipangwa kucheza na Ndovu ya Mwanza.
    Changanyikeni ya Dar es Salaam itacheza na Reha FC pia ya Dar es Salaam wakati Mshindi kati ya Kisarawe United na Silabu ya Mtwara atacheza na Kariakoo ya Lindi huku Cosmopolitan ikicheza na Ajabalo wakati Makumba FC itapambana na Green Warriors ya Kinondoni wakati Namungo FC ya Lindi itachuana na Villa Squad ya Dar es Salaam huku Dar City ikicheza na Majimaji Rangers ua Nachingwea.
    Michezo mingine ya hatua ya kwanza itakutanisha timu za Shupavu FC ya Morogoro na Sabasaba pia ya mjini humo wakati Motochini FC ya Katavi dhidi ya Ihefu FC ya Mbeya wakati The Mighty Elephant ya itacheza na Makanyagio ya Rukwa.
    Timu ya Burkina FC ya Morogoro itacheza na Mbinga United ya Ruvuma wakati Makambako Heroes ya Njombe  itacheza na Mkamba Rangers ya Morogoro wakati Real Moja Moja itapambana na African Wonderers – zote za Iringa. Boma FC ya Mbeya itacheza na African Sports ya Tanga.
    Mechi nyingine za hatua hiyo itakuwa ni kati ya Pepsi ya Arusha ambayo itacheza na Kilimanjaro Heroes ya Kilimanjaro; huku Stand Misuna ya Singida itacheza na Madini FC ya Arusha ilihali AFC ya Arusha itacheza na Nyanza ya Manyara wakati New Generation itacheza na Mshindi kati ya Usamala FC na Sahale ya Tanga. Bodaboda FC itacheza na Kitayose ya Kilimanjaro.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU 91 KUSHIRIKI AZAM SPORTS FEDERETION CUP, MICHUANO KUANZA NOVEMBA 7 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top