• HABARI MPYA

  Friday, October 06, 2017

  ARGENTINA NA MESSI HATARINI KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKANI URUSI BAADA YA SARE YA 0-0 NA PERU JANA NYUMBANI

  TIMU ya taifa ya Argentina na mchezaji wake mashuhuri, Lionel Messi wapo hatarini kuzikosa fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1970, kufuatia sare ya 0-0 nyumbani dhidi ya Peru mjini Buenos Aires.
  Imesalia raundi moja tu kukamilika kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Kundi la Amerika ya Kusini.
  Argentina, washindi wa pili wa Fainali za Kombe zilizopita za Kombe la Dunia baada ya kufungwa na Ujerumani katika fainali miaka mitatu iliyopita nchini Brazil, Jumanne watamenyana na Ecuador katika mchezo wa mwisho ugenini kwenye hewa nyembamba ya Quito mjini Andes.

  Lionel Messi akichezewa rafu na mchezaji wa Peru, Wilder Cartagena kwenye mchezo mgumu wa jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Kwa sasa Argentina inashika nafasi ya sita, na timu nne za juu ndizo zinazofuzu moja kwa moja fainali za mwakani Urusi. Mshindi wa tano anaweza kufuzu kwa kushinda mechi ya mchujo dhidi ya New Zealand. 

  Brazil tayari imefuzu hata kabla ya sare ya 0-0 jana dhidi ya Bolivia. Brazil ina pointi 38, ikifuatiwa na Uruguay pointi 28, Chile pointi 26 sawa na Colombia, Peru pointi 25 sawa na Argentina na Paraguay pointi 24.
  Ecuador, Venezuela na Bolivia hizo tayari zimetolewa.
  Mambo ni magumu, lakini Uruguay inatarajia kujihakikishia kufuzu Jumanne na baada ya hapo, timu nne zitakamata tiketi zake za Urusi.
  Zitaacha mzigo kwa timu mbili kuwania nafasi ya kufuzu kupitia mchujo na huko ndipo inaonekana Argentina wataibukia, lakini ni lazima washinde Quito ili wapate msaada.
  Kikosi cha Argentina kilikuwa; Romero, Mercado, Mascherano, Otamendi, Acuna, Banega/Gago dk61/Perez dk67, Biglia, Messi, Di Maria/Rigoni dk46, Alejandro Gomez na Benedetto.
  Peru: Gallese, Corzo, Araujo, Rodriguez, Trauco, Tapia/Aquino dk78, Pena/Cartagena dk53, Yotun, Farfan/Polo dk72, Guerrero na Flores.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARGENTINA NA MESSI HATARINI KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA MWAKANI URUSI BAADA YA SARE YA 0-0 NA PERU JANA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top