• HABARI MPYA

    Wednesday, August 09, 2017

    UNADHANI HARUNA ALISEMA NENO GANI HAPA KWA HASIRA JANA?

    Kiungo mpya wa Simba, Haruna Niyonzima akifoka kwa hasira baada ya kutia krosi nzuri, lakini wachezaji wenzake wakashindwa kuiunganishia nyavuni jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sport ya kwao, Rwanda kwenye mchezo wa kirafiki  
    Haruna aliingia kipindi cha pili na kucheza vizuri, ikiwa ni pamoja na kuseti nafasi za kufunga ambazo wachezaji wenzake walishindwa kuzitumia 
    Nafasi hii iliyomfanya akahamaki ndiyo iliyokuwa nzuri zaidi
    Lakini ajabu wachezaji watatu wa Simba walishindwa kuugusa mpira uingia nyavuni
    Haruna Niyonzima amehania Simba mwezi huu kutoka kwa mahasimu, Yanga  
    Pamoja na kukasirika na kutoa yowe kali, lakini Haruna Niyonzima aliinuka kuendelea na mchezo
    ingawa hata wakati anainuka alionekana bado ana hasira
    Na akaendelea kusema maneno kama kulalamika kwa waliopoteza nafasi hiyo
    Haruna Niyonzima anafahamika kama mchezaji mwenye hasira, ambazo wakati mwingine humponza kuonyeshwa kuonyeshwa kaid nyekundu
    Hii ndiyo krosi ya kitaalamu Haruna Niyonzima alipiga mpira ukaenda karibu kabisa lango ukihitaji mtu wa kuugusa tu uingie nyavuni
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UNADHANI HARUNA ALISEMA NENO GANI HAPA KWA HASIRA JANA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top