• HABARI MPYA

    Thursday, August 03, 2017

    MICHO AREJEA ORLANDO PIRATES, ATAMBULISHWA RASMI LEO

    KLABU ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imemrejesha kocha wake wa zamani, Mserbia Milutin Sredejovic 'Micho' kama kocha wake Mkuu tena.
    Mserbia huyo mwenye umri wa miaka 47 anaanza kazi mara moja na leo ametambulishwa.
    Akiwa ana umri wa miaka 37 tu, Micho aliwasili kwa mara ya kwanza Pirates na akaiongoza hadi Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Micho anarejea Pirates baada ya kuvunja mkataba na Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) kufundisha timu ya taifa ya nchi hiyo, The Cranes kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yake hadi kufika dola za Kimarekani 64, zaidi ya Sh. Milioni 140 za Tanzania. 

    Micho akiwa kwenye gari la wazi wakati wa kutambulishwa Orlando Pirates leo
    Micho akizungumza leo baada ya kutambulishwa leo Orlando Pirates

    Micho ambaye Septemba 1, mwaka huu atafikisha umri wa miaka 48 ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba anafurahi kurudi Pirates na ana matumaini ataendeleza rekodi yake nzzuri.
    Micho anaondoka Uganda baada ya miaka minne, akijivunia kuiwezesha The Cranes kurejea kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Januari mwaka huu nchini Gabon baada ya miaka 38.
    Kwa ujumla Micho ameiongoza Uganda katika mechi 85, zikiwemo sita za timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 na kati ya hizo 28 za ni kirafiki za kimataifa na 51 ni za mashindano.
    Katika mechi 51 za mashindano, wameshinda mara 29, sare 11 na kufungwa 11, lakini pamoja na mafanikio yote hiyo inasikitisha Micho amekuwa halipwi mishahara.
    Uganda ndiyo nchi ya kwanza Micho kufanya kazi barani Afrika akitokea moja kwa moja kwao, Serbia na kujiunga na klabu ya SC Villa mwaka 2001 alikodumu hadi 2004 alipohamia St. George ya Ethiopia ambako alifundisha hadi mwaka mwaka 2006 alipohamia Orlando Pirates.
    Baadaye mwaka huo akaenda kujiunga na Yanga SC ya Tanzania ambako baada ya miezi kadhaa akrudi Ethiopia kufundisha Saint-George hadi 2010 alipohamia Al-Hilal Omdurman ya Sudan alipodumu hadi 2011 alipokwenda kufungua ukurasa mpya taaluma yake, kufundishantimu za taifa akianza na wanda.
    Micho mshindi wa mataji 14 ya Ligi tofauti Afrika, mwaka 2013 aliondoka na Rwanda na kurudi Uganda, alipojiunga na The Cranes ambako aliendeleza mafanikio yake na kujijengea heshima kubwa.
    Haikuwa ajabu baada ya kuiwezesha The Cranes kurudi AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978, Micho akaingia kwenye kinyanganyiro cha tuzo ya kocha Bora Afrika, ambayo hata hivyo ilikwenda kwa Pitso Mosimane wa Mamelodi Sundowns, klabu bingwa Afrika, lakini Uganda ikachaguliwa timu bora ya Afrika.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO AREJEA ORLANDO PIRATES, ATAMBULISHWA RASMI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top