• HABARI MPYA

    Wednesday, August 09, 2017

    HANS POPPE: GYAN ATARUDI KUANZIA AGOSTI 20

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba mshambuliaji wao mpya, Nicholas Gyan ataondoka kurejea klabu yake, Ebusua Dwarfs ya kwao, Ghana ili kukamilisha taratibu za uhamisho wake.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Hans Poppe amesema kwamba, Gyan alilazimika kuja kushiriki tamasha la Simba Day ambalo ni maalum kwa utambulisho wa wachezaji wapya, lakini leo anarejea Ghana.
    Hans Poppe amesema kwamba Gyan anamaliza mkataba wake Agosti 20, mwaka huu Ebusua Dwarfs na baada ya hapo atarejea nchini – maana yake anaweza kuiwahi mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Yanga Agosti 23, mwaka huu.
    Mshambuliaji mpya, Nicholas Gyan kutoka Ebusua Dwarfs ya kwao, Ghana anaondoka na atarejea baada ya Agosti 20 kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uajili ya Simba, Zacharai Hans Poppe (pichani chini)
    Hans Poppe alikuwa mwenye furaha jana kuishuhudia timu yake ikizindua kikosi cha msimu mpya kizuri, chenye nyota wanaotarajiwa kuiwezesha timu hiyo kufufua ufalme wake kwenye soka ya Tanzania.         
    Hao ni pamoja na Agyei na Mghana mwenzake, kiungo James Kotei, beki Mzimbabwe na Nahodha Method Mwanjali, Waganda beki Juuko Murshid, mshambuliaji Emmanuel Okwi, kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima na mshambuliji Mrundi, Laudit Mavugo kwa upande wa wachezaji wa kigeni.
    Kwa upande wa wazawa ni Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jamal Mwambeleko, Salim Mbonde, Shiza Kichuya Muzamil Yassin, John Bocco, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Said Mohammed, Eamanuel Mseja, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Yussuf Mlipili, Ally Shomary, Jonas Mkude, Said Ndemla, Juma Luizio, Mwinyi Kazimoto na Jamal Mnyate.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HANS POPPE: GYAN ATARUDI KUANZIA AGOSTI 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top