• HABARI MPYA

    Monday, August 21, 2017

    DAKTARI WA TAIFA STARS YA MAXIMO AFARIKI DUNIA

    Na Salum Vuai, ZANZIBAR
    ALIYEWAHI kuwa daktari mkuu wa timu ya soka ya Taifa Tanzania, Taifa Stars Abdallah Said Mohammed al-maaruf ‘Kuku’, amefariki dunia usiku wa jana Agosti 20, 2017 nyumbani kwake Muembetanga mjini Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mfupi. 
    Marehemu alilitumikia benchi la ufundi Taifa Stars wakati kikosi hicho kikinolewa na Marcio Maximo kutoka Brazil na msaidizi wake Mzanzibari, Ali Bushiri, ambacho kilifanikiwa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
    Jeneza lililobeba mwili wa marehemu (katika picha ndogo kushoto) likitolewa msikiti maiti, Michenzani baada ya kusaliwa kuelekea malazoni. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake pahala pema Peponi. Amin.

    Aidha aliwahi kuwa daktari wa timu ya taifa ya vijana U-20 wakati huo ikiitwa Karume Boys.
    Marehemu amezikwa leo mchana kijijini kwao Fujoni Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, ambapo mazishi yake yalihudhuriwa na mamia ya wananchi wa Zanzibar wakiwemo wanamichezo, madaktari na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali alizozifanyia kazi ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) akihudumu katika kiwanja cha kufurahisha watoto Kariakoo kilicho chini ya mfuko huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DAKTARI WA TAIFA STARS YA MAXIMO AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top