• HABARI MPYA

  Tuesday, July 18, 2017

  LUKAKU AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO MAN UNITED IKICHINJA 2-1

  Mshambuliaji mpya wa Manchester United, Romelu Lukaku akimuacha chini kipa wa Real Salt Lake, Eduardo Fernandez baada ya kumzunguka na kuifungia timu yake bao la pili dakika ya 38 Uwanja wa Rio Tinto, Sandy, Utah, Marekani katika ushindi wa 2-1. Hilo linakuwa bao la kwanza kabisa kwa Lukaku tangu ajiunge na Mashetani hao Wekundu wiki mbili zilizopita kwa dau la rekodi, Pauni Milioni 75 kutoka Everton, zote za England. Bao la kwanza la United kwenye mchezo huo wa alfajiri hii limefungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika ya 29, baada ya Luis Silva kuitanguliza Real Salt Lake dakika ya 23  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO MAN UNITED IKICHINJA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top