• HABARI MPYA

  Tuesday, July 18, 2017

  'DOGO' MSENEGALI ALAMBA MKATABA WA MIAKA MITATU LYON

  KIUNGO mshambuliaji wa Senegal, Ousseynou Ndiaye amesaini mkataba wa mitatu kujiunga na timu ya Ligue 1 Ufaransa, Olympique Lyonnais.
  Mchezaji huyo kijana wa umri wa miaka 18 alisaini mkataba huo jana kutoka Diambars FC de Saly, ambayo ni akademi ya soka nchini Senegal.
  Ndiaye amevutiwa mno na kusajiliwa na klabu hiyo ya Ligi daraja la juu zaiid Ufaransa na ana matumaini ya kuwa mfano.
  Pamoja na hayo, amekiri bado ana safari ndefu ya kwenda."Nina furaha sana kusaini OL. Ni klabu kubwa. Ni ndoto kuwa hapa. Nataka kuwa mfano kwa watu niliowaacha nyuma Senegal. Si rahisi kupata kupata mkataba wa mwanasoka wa kulipwa. Bado kuna hatua nyingi mbele yangu," alisema Ndiaye.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'DOGO' MSENEGALI ALAMBA MKATABA WA MIAKA MITATU LYON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top