• HABARI MPYA

  Monday, July 10, 2017

  CRISTIANO RONALDO AAMUA KUBAKI REAL MADRID

  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amebadilisha mawazo yake na kuamua kubaki Real Madrid, kwa mujibu wa taarifa nchini Hispania.
  Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amekiri Ronaldo 'aliumizwa na kukasirika' kutokana na madai ya Mamlaka ya Hispania kwamba alikwepa kosi ya Pauni Milioni 12.9.
  Ronaldo aliiambia klabu kwamba angeondoka ikiwa atatiwa hatiani kwa mashitaka ya kukwepa kodi na pia alifanya kikao cha siri na Rais wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi, saa kadhaa kabla ya kufunga mabao mawili kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus.
  Ureno ya Cristiano Ronaldo ilitolewa katika Nusu Fainali Kombe la Mabara na Chile PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Lakini AS limerip[oti kwamba Ronaldo sasa ameamua kubaki Madrid, baada ya kushawishiwa na klabu kwamba bado ni mtu muhimu katika mipango yao ya baadate.
  Kesi ya Ronaldo kukwepa kodi inatarajiwa kuunguruma mahakamani Julai 31, ingawa wawakilishi wake sasa wanampoza mambo hayatakuwa magumu.
  Awali Perez alisema atazungumza na mchezaji huyo atakaporejea kutoka kwenye Kombe la Mabara huku akiamini atabaki.
  Rais huyo alirudia kusema kwamba Ronaldo hakufanyiwa mambo ya kiungwana kutokana na nyota wake huyo 'kuchukuliwa kama mhalifu'. 
  Ronaldo amerejea Madrid ndani ya muda kuungana na wanawe wapya pacha wawili waliozaliwa kwa mama asiyejulikana, baada ya Ureno kutolewa Nusu Fainali kwenye Kombe la Mabara na Chile. 
  Ingawa kikosi cha Madrid kinaripoti leo kwa maandalizi ya msimu mpya, Ronaldo atapewa muda zaidi wa mapumziko kuimarika zaidi na hatarajiwi kurudi hadi mwishoni mwa Julai.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CRISTIANO RONALDO AAMUA KUBAKI REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top