• HABARI MPYA

  Friday, June 16, 2017

  YANGA YAIPA ‘ZA CHEMBE’ SIMBA, YAMSAINI BUSWITA MIAKA MIWILI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imeonyesha haiwezi kuzidiwa ujanja na mahasimu Simba kwa mchezaji yeyote wamtakaye, baada ya leo kufanikiwa kumsaini kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC ya Mwanza.
  Juzi, Simba walitamba kumalizana na kiungo huyo anayeweza kucheza kama winga na mshambuliaji pia wakati tayari tetesi zilikuwa zimezagaa kwamba yuko kwenye rada za Yanga. 
  Lakini baada ya ukimya wa saa 24, Yanga wanaibuka na jibu la kuwafunga kabisa mdomo mahasimu wao, Simba wakiwa wameingia mkataba na miaka miwili na mchezaji huyo aliyeng’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita.
  Pius Buswita (kushoto) akitia dole gumba kwenye fomu za Yanga. katikati ni Mhasibu wa klabu, Baraka Deusdedit 
  Pius Buswita akitamba na mpira katikati ya wachezaji wa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam

  Rasmi huyo anatakuwa mchezaji wa pili kusajili Yanga baada ya beki wa Taifa ya Jang’ombe, Abdallah Hajji Shaibu, lakini habari zisizo rasmi zinasema hata kipa Mcameroon, Youthe Rostand naye amesaini ingawa haujapatikana uthibitisho wowote hadi sasa.
  Wengine wanaotajwa kuwa kwenye mpango wa kusailiwa Yanga ni Babu Ally Seif kutoka Kagera Sugar, Ibrahim Hajib kutoka Simba na Himid Mao kutoka Azam FC.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAIPA ‘ZA CHEMBE’ SIMBA, YAMSAINI BUSWITA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top