• HABARI MPYA

  Thursday, June 15, 2017

  VIGOGO WAWILI TFF WABWAGA MAPEMAAA KISA WANAJUA WENYEWE

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  WAJUMBE wawili wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ahmed 'Msafiri' Mgoyi na Wilfred Kidau wamejitoa mapema kwenye mbio za uchaguzi za shirikisho hilo Agosti 12, mwaka huu.
  Mapema wiki hii, TFF imetangaza kuanza rasmi mchakato wa uchaguzi wa shirikisho hilo kwa kutaja tarehe ya kuanza fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ambayo ni Juni 16 hadi Juni 20, mwaka huu katika ofisi zake zilizopo Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, huku wachukua fimu wakitakiwa kuzilipia katika benki ya CRDB kupitia akaunti namba 01J1019956700.
  Gharama za kuchukulia fomu ni Sh. 500,000 kwa nafasi ya Urais, Sh. 300,000 kwa Makamu wa Rais na Sh. 200,000 nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji na baada ya kulipia benki watatakiwa kupeleka risiti TFF.
  Wilfred Kidau (kulia) akiwa na Ahmed Iddi Mgoyi, maarufu kama Msafiri (kushoto)

  Wakati mchakato ukianza rasmi, Mgoyi na Kidau waliokuwa ‘wajumbe wazito’ wametoa taarifa ndefu leo, wakisema hawatagombea. 
  “Pamoja na kuwa bado nina nguvu uwezo na sifa za kuendelea kugombea, lakini pia nimeamini ni wakati wa kutoa nafasi pana zaidi kwa wengine kugombea na kuwa badala yangu na heshima kwa fikra nyinginezo. Na ninaondoka nikiwa mjumbe wa muda mrefu zaidi ya wote kwenye Kamati ya Utendaji inayokamilisha kipindi cha kikatiba na kwa dhati kabisa naamini kwenye kutoa nafasi kwa wengine,”amesema Na Mgoyi na kuongeza.
  “Nawaomba radhi wale wote ambao wangependa au kutarajia ningekuwa miongoni au wakiendelea kuamini kuwa nilistahili kuwa sehemu ya wagombea.. nawashukuru kwa imani yao kwangu na bado nipo nao pamoja, pamoja na wale ambao hawaamini hivyo kama sehemu ya familia ya Mpira wa Miguu Tanzania na kwingineko,”.
  Mbali na Mgoyi ambaye amekuwa Mjumbe Kamati ya Utendaji TFF akiiwakilisha mikoa Kigoma na Tabora tangu mwaka 2004, Kidau naye kwa upande wake amesema; “Wajumbe waliona kwa sifa hizi na nyingine ambazo sijaziweka, bado mchango wangu unahitajika sana ndani ya Kamati ya Utendaji ya TFF, hususan kwenye maeneo ya Ufundi na ushauri juu ya taratibu za manunuzi nilipobobea,:”.
  “Lakini baada ya kutafakari sana, niwaombe radhi ndugu zangu Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, hasa wale waliosema wapo tayari kunipigia kampeni  kwa hali na mali, kwamba sitagombea uongozi.Naamini wapo watakaoumizwa na hili, lakini yote ni kwa maslahi mapana ya mpira wetu,”.
  Kidau amesema ameona ni wakati muafaka kwake kupata changamoto za kuusaidia mpira nje ya Kamati ya Utendaji ya TFF. “Ninaweza kuwa sahihi au nikawa nimekosea, lakini kuwa na uhuru wa kuamua ndio kitu ninachokipenda kwenye maisha yangu na sitaki kubadili hilo,”.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIGOGO WAWILI TFF WABWAGA MAPEMAAA KISA WANAJUA WENYEWE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top