• HABARI MPYA

  Saturday, June 17, 2017

  RONALDO KUONDOKA REAL MADRID KUKIMBIA 'MSALA' WA KODI

  MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameamua kuondoka Real Madrid baada ya kuwaambia wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ureno nia yake, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
  Mustakabali wa Ronaldo Real Madrid haueleweki kutokana na mshambuliaji huyo kusema hana furaha kufuatia kesi ya kukwepa kodi Hispania, Pauni Miklioni 13. Ameionya klabu hiyo ataondoka iwapo atatiwa hatiani.
  Na gazeti la la Marca la mjini Madrid limesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atafanya hivyo baada ya kuwaeleza wachezaji wenzake wa timu ya taifa mipango yake.

  Cristiano Ronaldo (katikati) amewaambia wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ureno anaondoka Real Madrid PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  Ronaldo kwa sasa yuko Urusi na kikosi cha Ureno kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mabara Confederations kujaribu kurudia mafanikio yao ya Euro 2016 nchini Ufaransa.
  Nukuu katika gazeti la Marca inasema kwamba Ronaldo amewaambia wachezaji wenzake: "Ninaondoka Real Madrid. Nimefanya maamuzi. Hakuna kurudi nyuma.'
  Paris Saint-Germain ikitajwa kama klabu ya kwanza ambayo mchezaji huyo anaweza kujiunga nayo, inatarajiwa kuanza rasmi kuifukuzia saini ya Cristiano Ronaldo kama mshindi huyo wa Ballon d'Or nne ataondoka Real baada ya msimu mzuri akiiachia taji la La Liga na Ligi ya Mabingwa.
  Manchester United ingependa kumrejesha nyota huyo Mreno huyo Old Trafford, lakini kwanza wanatakiwa kuchunguza baada ya taarifa ya kufanyika kikao cha siri kati ya wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes na Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi mjini Cardiff mchana kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa.
  Inafahamika Mendes amemuambia Al-Khelaifi juu ya matatizo hayo yanavyozidi kukuwa na amemuahidi kuendeleakuwasiliana kupeana taarifa zaidi.
  PSG imekuwa ikimfukuzia mwenye umri wa miaka 32 kwa miaka sasa itakuwa tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili kumpata Ronaldo.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO KUONDOKA REAL MADRID KUKIMBIA 'MSALA' WA KODI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top