• HABARI MPYA

  Monday, June 05, 2017

  NGASSA APANGULIWA SPORTPESA SUPER CUP

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Mashindano ya SportPesa Super Cup imemzuia kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Mrisho Khalfan Ngassa kuichezea timu yake ya zamani, Yanga SC katika michuano hiyo.
  Yanga inaanza kuwania Kombe hilo linaloambatana na zawadi ya zaidi ya Sh. Milioni 65 za Tanzania kwa kumenyana na Tusker FC ya Kenya kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Na leo ilipanga kumtumia Ngassa, lakini saa chache kabla ya kwenda kwenye uwanjani, ikapewa taarifa haiwezi kumtumia mchezaji huyo, vinginevyo iwe na mkataba naye au barua maalum ya ruhusa kutoka klabu yake, Mbeya City.
  Kwa sababu hiyo, kocha anayeiongoza Yanga katika mashindano haya, Juma Mwambusi baada ya bosi wake, Mzambia, George Lwandamina kwenda nyumbani, Kenya kwa mapumziko akapangua kikosi.
  Kikosi ch Yanga sasa kinachoanza leo ni; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Emmanuel Kichiba, Andrew Vincent ‘Dante’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Babu Ally, Yussuf Mhilu, Maka Mwakalukwa, Obrey Chirwa, Juma Mahadhi na Emmanuel Martin. 
  Katika benchi wapo Bakari Osman, Mohamed Ally, Rahim Shea, Said Mussa, Samuel Greyson na Pato Ngonyani.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA APANGULIWA SPORTPESA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top