• HABARI MPYA

    Monday, June 05, 2017

    SAKHO WA LIVERPOOL ATUA MOSHI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

    Na Mwandishi Wetu, KILIMANJARO
    BEKI wa kimataifa wa Ufaransa, Mamadou Sakho anayechezea Liverpool ya England yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kiutalii.
    Sakho ameonekana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo na inafikiriwa anakwenda kupanda mlima Kilimanjaro.
    Mchezaji huyo anaonekana Tanzania siku mbili tu baada ya Nahodha na kiungo wa zamani wa kimataifa wa England, David Beckham kuondoka nchini kufuatia wiki moja ya kutalii kwenye vivutio mbalimbali, ikiwemo mbuga ya wanyama ya Serengeti.
    Mamadou Sakho (katikati) akiwa na wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya kuwasili kwa ziara ya utalii 

    Sakho aliyezaliwa Februari 13, mwaka 1990, kisoka aliibukia Paris FC kabla ya kuhamia timu ya vijana ya Paris Saint-Germain mwaka 2002 na Oktoba mwaka 2007 aliweka rekodi ya mchezaji kijana daima kuiongoza timu hiyo kam Nahodha katika Ligue 1. 
    Sakho amecheza mechi zaidi ya 200 katika klabu hiyo, akishinda nayo mataji yote manne ya nyumbani kabla ya mwaka 2013 kuuzwa Liverpool kwa dau la Pauni Milioni 18.
    Mwaka huu alitolewa kwa mkopo Crystal Palace pia ya Ligi Kuu England ambako amekwenda kucheza mechi nane.
    Sakho ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha wakubwa cha Ufaransa, ambaye awali amechezea timu zote za vijana na za nchi hiyo.
    Mamadou Sakho (kulia) akizungumza na kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp (kushoto)

    Tangu acheze mechi yake ya kwanza kikosi cha wakubwa cha Ufaransa mwaka 2010 dhidi ya England, Sakho amecheza mechi zaidi ya 25 na alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye Fainali za Kombe la Dunia  mwaka 2014 nchini Brazil.
    Huyo ni mume wa Majda, ambaye amezaa naye watoto wawili wa kike, waliozaliwa mwaka 2013 na 2015. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAKHO WA LIVERPOOL ATUA MOSHI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top