• HABARI MPYA

  Friday, June 16, 2017

  MOURINHO AENDEA MBIO SAINI YA WINGA HATARI WA INTER MILAN

  TIMU ya Manchester United inataka kumsajili winga wa Inter Milan, Ivan Perisic kwa dau la Pauni Milioni 44 wiki za karibuni. 
  Jose Mourinho anaona winga huyo wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 28 ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa kusajili katika mkakati wa kuimarisha kikosi chake angalau kwa kuongeza nyota wapya wanne.
  Hakuna ada iliyokubaliwa, lakini makubaliano ya kimikataba yamefikiwa baina ya klabu hizo na Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu kwamba Mreno huyo anamtaka Perisic katika kikosi chake haraka kwa ajili ya ziara ya Marekani mwezi ujao.

  Jose Mourinho anamtaka haraka winga Ivan Perisic kutoka Inter Milan ya Italia katika harakati za kuimarisha kikosi chake cha Old Trafford PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Tayari Mourinho amemsajili beki wa Benfica, Victor Lindelof kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 30.7, dili ambalo lilikamilika Jumatano.
  Pia anataka kumuongeza mshaambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata achukue nafasi ya Zlatan Ibrahimovic, lakini kuna wasiwasi Old Trafford kwamba mpango wowote wa kumsajili mshambuliaji huyo utaifanya klabu ya Hispania nayo iombe kumsajili kipa wao, David de Gea, mchezaji ambaye hawataki kumpoteza.
  Kiwango cha kipa wao wa sasa, Keylor Navas kimeibua taarifa kwamba Real Madrid imeachana na mpango wa kumfuatilia De Gea, aliyekaribia kujiunga na timu hiyo ya La Liga mwaka 2015 kabla ya kukwama dakika ya mwisho.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOURINHO AENDEA MBIO SAINI YA WINGA HATARI WA INTER MILAN Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top