• HABARI MPYA

  Saturday, June 03, 2017

  ZIDANE: RONALDO NI BORA KULIKO MIMI WAKATI WANGU

  KOCHA wa Real Madrid ya Hispania, Zinedine Zidane amesema kwamba Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri kuliko alivyokuwa yeye enzi zake.
  Zidane anatumaini Ronaldo ataiongoza Real kutwaa tena taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo, itakapomenyana na Juventus ya Italia mjini Cardiff usiku wa Jumamosi.
  Ronaldo amefunga jumla ya mabao 49 kwa klabu na nchi yake msimu huu na amefunga hat-tricks (mabao matatu katika mchezo mmoja) kwenye hatua zote, Robo Fainali na Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa.


  Zinedine Zidane akifurahia na Cristiano Ronaldo baada ya kushinda taji PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Alipoulizwa katika mkutano na Waandishi wa Habaru, nani angekuwa bora kama wawili hao wangecheza zama moja, mshambuliaji gwiji wa Ufaransa Zidane, akasema: "Ronaldo, hakuna shaka.
  "Anafunga mabao na hilo ndilo muhimu zaidi. Nilikuwa nacheza vizuri mno, lakini kufunga mabao siku mtu maalum. Nilikuwa mzuri katika kutengeneza nafasi za mabaoa. Nilifunga mabao fulani muhimu, lakini si megi kama yeye,'alisema.
  Zidane alizichezea zote, Real na Juventus enzi za ujana wake.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE: RONALDO NI BORA KULIKO MIMI WAKATI WANGU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top