• HABARI MPYA

  Friday, June 02, 2017

  KHAMIS MCHA ''VIALLI' ATUPIWA VIRAGO AZAM FC

  Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Azam FC, umeweka wazi kimtema mchezaji wake Khamis Mcha 'Vialli', baada ya kumaliza mkataba wake na timu hiyo.
  Akizungumza na Waandishi wa habari, Ofisa habari wa Azam, Jaffer Iddi alisema benchi la ufundi limetoa repoti ya kutoendelea na mchezaji huyo.
  Alisema mbali na mchezaji huyo pia Ame Ally amemaliza mkataba na hawataendelea tea.
  Ame ambaye alikwenda kwa mkopo Simba na msimu huu kucheze Kagera Sugar ambao wamemaliza Ligi Kuu Tanzania Bara.
  Khamis Mcha 'Vialli' ametemwa Azam FC baada ya kumaliza mkataba wake 

  "Kwa sasa wachezaji hao sio wa Azam na kuitakia baraka huko waendako, pia suala la Aishi Manula na Shomari Kapombe wako katika mazungumzo," alisema.
  Jaffer alisema wachezaji hao wakitoka katika kikosi cha Taifa Stars watakaa meza moja na kusaini mikataba mipya.
  Alisema katika usajili mpya alisema wanakuwa makini katika usajili wa wachezaji wa ndani kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi.
  " Mazoezi tunaanza rasmi Julai 9 mwaka huu na timu tutakaa katika hostel zetu zilizopo Chamazi, hatutakwenda nje ya nchi," alisema
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KHAMIS MCHA ''VIALLI' ATUPIWA VIRAGO AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top