• HABARI MPYA

  Thursday, June 01, 2017

  KIUNGO FUNDI WA MBAO ‘AZICHONGANISHA’ SIMBA NA YANGA

  Na Shekha Jamal, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Salmin Hoza wa Mbao FC, amesema kwamba atakayefika na dau nzuri kati ya Simba na Yanga au timu nyingine yoyote, ndiye atakayepata saini yake.
  Zote, Simba na Yanga zimeripotiwa kuwania saini ya kiungo huyo aliyeng’ara msimu huu akiwa na kikosi cha Mbao FC, lakini akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Hoza amesema yeye anaangalia maslahi tu. 
  Amesema amemaliza mkataba wake Mbao FC na hajaongeza akiwa bado anasubiri kulinganisha ofa atakazoletewa ndipo afanye maamuzi.

  Salmin Hoza (kulia) anazikaribisha Simba na Yanga kwa mazungumzo ya kumng'oa Mbao FC 

  “Sijapokea taarifa rasmi ya kutakiwa na timu yoyote, zaidi ya kusikia tu kwenye vyombo vya habari kwamba Simba na Yanga wananifuatilia,”alisema.
  Hoza ambaye anavutiwa sana na uchezaji wa kiungo wa Simba, Said Ndemla amesema milango iko wazi kwa timu yoyote inayomtaka.
  Pamoja na kucheza vizuri katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini pia Hoza aling’ara katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Mbao FC ikifungwa 2-1 na Simba ndani ya dakika 120.
  Na baada ya mchezo, jina lake likazidi kuvuma kama miongoni mwa wachezaji ambao ni vigumu kubaki Mbao FC kutokana na kiwango kizuri walichoonyesha kwamba kitazivutia timu kubwa na kugombea saini yake.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO FUNDI WA MBAO ‘AZICHONGANISHA’ SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top