• HABARI MPYA

  Friday, June 02, 2017

  GRIEZMANN AWAGEUKA MAN UNITED, AAMUA KUBAKI MADRID

  MSHAMBULIAJI Antoine Griezmann ameamua kubaki Atletico Madrid msimu ujao na kumaliza tetesi za kuhamia Manchester United kwa dau la Pauni Milioni 86.
  Mpachika mabao huyo wa Kifaransa, kwa kiasi kikubwa amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford, lakini baada ya Atletico kufungiwa kusajili wachezaji wapya inaonekana amemaliza tetesi hizo.
  Jana jioni kwenye ukurasa wake wa Twitter, Griezmann aliweka picha yake akiwa amevaa jezi ya Atletico ikiwa imeambatana na maelezo yasemayo: "Sasa zaidi kuliko daima#Atleti #WotePamoja'

  Antoine Griezmann anatarajiwa kubaki Atletico Madrid maana yake hatakwenda tena Manchester United PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Tayari Man United imekwishasitisha mpango wa kumchukua mchezaji huyo na kuanza kuangalia namba 9 mwingine, huku wachezaji kama Romelu Lukaku wa Everton na Alvaro Morata wa Real Madrid wakipewa nafasi ya kuziba pengo la mkongwe Zlatan Ibrahimovic.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GRIEZMANN AWAGEUKA MAN UNITED, AAMUA KUBAKI MADRID Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top