• HABARI MPYA

    Friday, June 02, 2017

    SANGA: HAKUNA MCHEZAJI TUNAYEMTAKA ATAONDOKA YANGA, NA WOTE TUNAOWATAKA KUTOKA TIMU NYINGINE TUTAWAPATA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KAIMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amesema kwamba kila kitu kinakwenda sawa Yanga SC na hakuna mchezaji wanayemtaka ataondoka na wote wanaowahitaji kuboresha kikosi chao watawapata.
    Katika mahojiano maalum na Bin Zubeiry Sports – Online jana usiku, Sanga alisema kwamba baada ya kumaliza msimu, viongozi wamegawana majukumu katika kutekeleza masuala mbalimbali ya ustawi wa klabu kuelekea msimu ujao.
    Sanga amesema kwamba Kamati ya Mashindano imejikita kwenye suala la usajili kwa sasa na mchakato unaendelea vizuri, wakati Kamati nyingine zinaendelea na majukumu yake mengine pia.
    Clement Sanga amesema hakuna mchezaji wanayemtaka ataondoka na wote wanaowahitaji kuboresha kikosi chao watawapata

    “Nataka nikuhakikishie, kila kitu kinakwenda sawa Yanga na wachezaji wote tunaowahitaji wabaki, watabaki, hakuna atakayeondoka. Na ambao hatutaki, basi wataondoka,”alisema.
    Sanga pia amethibitisha kocha Mkuu, George Lwandamina kutoka Zambia ataendelea na kazi kwa msimu mwingine wa pili.
    Na kuhusu habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba mkataba wa udhamini wa SportPesa una kasoro kubwa, Sanga amesema si kweli.
    “Mkataba unaozunguka si mkataba ambao upo mikononi mwa Yanga, kama kuna mtu ambaye ni mwanachama anaweza kupita makao makuu ya klabu (Jangwani, Dar es Salaam) kwa Katibu (Charles Boniface Mkwasa) nimemwagiza awaruhusu watu kuuona ukiwa pale,”alisema. 
    Pamoja na hayo, Sanga amesema kwamba klabu inahitaji utulivu sana kipindi hiki, wakati viongozi wanaendelea kuweka mambo mengi sawa.
    Na akasema Mwenyekiti Manji amejiuzulu kwa wema tu na hata kinyongo na mtu yeyote wala klabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SANGA: HAKUNA MCHEZAJI TUNAYEMTAKA ATAONDOKA YANGA, NA WOTE TUNAOWATAKA KUTOKA TIMU NYINGINE TUTAWAPATA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top