• HABARI MPYA

  Wednesday, April 12, 2017

  YANGA KUWAFUATA MC ALGER ALHAMISI BILA ZULU

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA SC inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Alhamisi kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Mouloudia Club Alger Jumamosi Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers.
  Mabingwa hao wa Tanzania wataendelea kumkosa kiungo wao Mzambia, Justin Zulu aliyeumia Aprili 1, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa aliiambia Bin Zubeiry Sports – Online jana  kwamba wanamtarajia Zulu kuanza mazoezi mepesi leo na hayumo kabisa kwenye mipango ya mchezo wa marudiano dhidi ya MC Alger.
  Kuhusu orodha ya wachezaji watakaokwenda Algeria, Mkwasa alisema itajulikana baada ya mazoezi ya leo jioni.
  Yanga iliyoshinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, inahitaji kwenda kulazimisha sare tu ugenini ili kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu.
  Mwaka jana, Yanga pia ilicheza hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola ikitoka kutolewa na Al Ahly ya Misri katika Ligi ya Mabingwa.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUWAFUATA MC ALGER ALHAMISI BILA ZULU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top