• HABARI MPYA

    Wednesday, April 12, 2017

    SERENGETI BOYS WAENDELEA NA MAKAMUZI RABAT

    Na Mwandishi Wetu, RABAT
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeendelea na mazoezi katika kambi yake ya Kituo cha Taifa cha Soka Maamoura Mjini Rabat Nchini Morocco kujiandaa na Fainali za U-17 Afrika mwezi ujao nchini Gabon.
    Serengeti Boys ipo Rabat tangu Aprili 5, ilipowasili kwa kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na michuano ya Gabon baada ya mechi tatu za kujipima nguvu nyumbani, dhidi ya Burundi mara mbili wakishinda 3-0 na 2-0 na dhidi ya Ghana wakitoka sare ya 2-2.
    Serengeti itakuwa huko hadi Mei watakapokwenda Younde, Cameroon kwa maandalizi ya mwisho mwisho ikiwemo michezo miwili ya kirafiki dhidi ya wenyeji, Mei 3 na 6, mwaka huu kupima uwezo wa timu kabla ya Mei 7 kwenda Gabon ambako Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola.
    Kikosi cha Serengeti Boys kilichopo Rabat kinaundwa na Makipa:  Ramadhan Kabwili, Samwel Edward na Kelvin Kayego. 
    Beki: Kibwana Ally Shomari, Nickson Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick Vitalis Nkosi. 
    Viungo: Kelvin Nashon Naftali, Ally Ng’anzi, Mohamed Rashid, Shaaban Ada, Mathias Juan, Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman, Saidi Mussa na Cyprian Benedictor Mtesigwa.
    Washambuliaji:  Muhsin Malima Makame, Yohana Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.
    Benchi la Ufundi linaundwa na Bakari Shime (Kocha Mkuu), Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi), Muharami Mohamed (Kocha wa makipa), Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi), Edward Evans (Mtunza Vifaa) na Shecky Mngazija (Daktari wa timu).
    Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zinatarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28 Mwaka huu Nchini Gabon na Tanzania iliyopo kundi B itafungua Dimba Mei 15 na Mali kabla ya Mei 18 kuwakabili Angola na baadaye kumaliza na Niger.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAENDELEA NA MAKAMUZI RABAT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top