• HABARI MPYA

    Saturday, April 15, 2017

    SIMBA YAKWAMA KWA TOTO LA YANGA, SARE 0-0

    Na Steven Kinabo, MWANZA
    SIMBA SC imekwama leo, baada ya kuambulia sare ya 0-0 mbele ya wenyeji Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
    Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Simba ikifikisha pointi 62 pamoja na zile tatu za mezani walizopewa kwa madai Mohammed Fakhi alicheza akiwa ana kadi tatu za njano baada ya kufungwa na Kagera Suagr 2-1.
    Maana yake Simba SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi. 
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo wa Mara, aliyesadiwa na Hassan Zani wa Arusha na Abdallah Mkomwa wa Pwani dakika 45 za kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu.
    Frederick Blagnon (kulia) ameshindwa kuisaidia Simba leo mbele ya Toto Africans mjini Mwanza (Picha ya Maktaba) 

    Kulikuwa na kosa kosa pande zote mbili upande wa Simba Muivory Coast, Frederick Blagnon akipoteza nafasi ya wazi na kwa Toto, Nahodha Reliant Lusajo Mwakasagule naye akipoteza.
    Kipindi cha pili kocha Mcameroon wa Simba, Joseph Omog alianza kwa mabadiliko mfululizo akiwatoa kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na mshambuliaji Laudit Mavugo na kuwaingiza kiungo Mwinyi Kazimoto na mshambuliaji Ibrahim Hajib.
    Pamoja na mabadiliko hayo, mchezo uliendelea kuwa mgumu na Omog akaamua kumtoa na winga Shiza Ramadhani Kichuya na kumuingiza mshambuliaji Juma Luizio Ndanda, wakati kocha wa Toto, Furgence Novatus alimtoa Jamal Soud Mtengeta na kumuingiza Hamad Nathaniel Mbumba. 
    Bado mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili na refa Adongo akaongeza dakika tano kufidia muda uliopotezwa. Toto inafikisha pointi 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14 ikiishusha Maji Maji nafasi ya 15.
    Kikosi cha Toto Africans leo kilikuwa; Mwasa Kirungi, Juvenary Pastory, Ramadhani Malima, Hamim Abdul, Yussuf Mlipili, Carlos Kirenge, Jamal Mtengeta/Hamad Mbumba dk75, Hussein Kasanga, Waziri Junior, Reliant Lusajo na Jaffar Mohammed. 
    Simba SC; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Juuko Murshid, James Kotei, Shiza Kichuya/Juma Luizio dk76, Muzamil Yassin, Frederick Blagnon, Laudit Mavugo/Ibrahim Hajib dk58 na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Mwinyi Kazimoto dk54.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA YAKWAMA KWA TOTO LA YANGA, SARE 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top