• HABARI MPYA

  Saturday, April 15, 2017

  NGOMA ANAANZA, TAMBWE BENCHI YANGA NA MC ALGER LEO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amemuanzisha Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma kama mshambulaji pekee katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania tiketi ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Mouloudia Club Alger Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Al-Jaza’ir, Algiers.
  Katika mchezo huo utakaoanza Saa 12:00 jioni kwa Saa za Algeria na Saa 2:00 kwa Saa za Tanzania, Lwandamina amefanya mabadiliko pia kwenye safu ya ulinzi akiwaanzisha pamoja Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika beki ya kati. 
  Donald Ngoma anaanza leo dhidi ya Mouloudia Club Alger Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Al-Jaza’ir 

  Kwa ujumla kikosi cha Yanga leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Haruna Niyonzima na Deus Kaseke.
  Katika benchi wapo Beno Kakolanya, Juma Abdul, Juma Mahadhi, Emmanuel Martin, Amissi Tambwe, Andrew Vincent ‘Dante’ na Geoffrey Mwashiuya.
  Yanga ilishinda 1-0 mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na leo itahitaji sare tu ili kwenda hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya pili mfululizo. 
  Mwaka jana pia, Yanga pia ilicheza hatua ya makundi ya michuano hiyo baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola ikitoka kutolewa na Al Ahly ya Misri katika Ligi ya Mabingwa. 
  Na Lwandamina ana matumaini sana ya kumalizia vizuri mchezo wa leo na kusonga mbele, akijivunia rekodi ya kutopoteza mechi hata moja hadi sasa kwenye michuanio ya Afrika akitoa sare tatu na kushinda mmoja.
  Kila la heri Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGOMA ANAANZA, TAMBWE BENCHI YANGA NA MC ALGER LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top