• HABARI MPYA

  Thursday, April 06, 2017

  SIMBA YAIKATIA RUFAA KAGERA SUGAR, YADAI FAKHI ALICHEZA ANA KADI TATU ZA NJANO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC wamewasilisha rufaa Bodi ya Ligi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudai pointi za mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Jumamosi iliyopita.
  Simba iliyofungwa 2-1 na wenyeji wao hao katika mchezo huo wa Ligi Kuu, imedai kwamba Kagera walimchezesha beki Mohammed Fakhi akiwa ana kadi tatu za njano.
  Habari za ndani kutoka Simba zimesema kwamba mchezaji huyo alionyeshwa kadi katika kila mechi kati ya tatu mfululizo kabla ya kukutana na Wekundu wa Msimbazi na kwa mujibu wa kanuni hakuopaswa kushiriki mchezo wa Aprili 2.
  Mohammed Fakhi anadaiwa kucheza dhidi ya Simba akiwa ana kadi tatu za njano

  Wakati Kamati ya Saa 72 ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Tanzania inatarajiwa kukutana kesho, Kagera Sugar wametoa angalizo dhidi ya malalamiko ya Simba.
  Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema kwamba Fakhi alikuwa huru kucheza mechi dhidi ya Simba kwa sababu alikuwa ameonyeshwa kadi mbili tu za njano.
  “Mimi niko makini sana na masuala ya kadi ya wachezaji wangu. Kila mchezaji wangu anapoonyeshwa kadi naandika. Fakhi hakuwa na kadi tatu, Simba kama wameshindwa mpira uwanjani wasikimbilie kutafuta ushindi wa mezani kimizengwe,”alisema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAIKATIA RUFAA KAGERA SUGAR, YADAI FAKHI ALICHEZA ANA KADI TATU ZA NJANO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top