• HABARI MPYA

  Monday, April 17, 2017

  SAMATTA APUMZISHWA GENK IKISHINDA 3-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana alikuwa benchi kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya KV Kortrijk katika mchezo kuwania tiketi ya kucheza UEFA Europa League msimu ujao Uwanja wa Guldensporen, Kortrijk.
  Mabao ya Celta Vigo yalifungwa na kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy dakika ya 34, beki wa Gambia, Omar Colley na kiungo wa Ghana, Bennard Yao Kumordzi dakika ya 77.
  Bila shaka Samatta amepumzishwa kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Europa League dhidi ya Celta de Vigo ya Hispania Alhamisi wiki hii, Genk ikihitaji ushindi hata wa 1-0 kwenda Nusu Fainali baada ya kufungwa 3-2 kwenye mchezo wa kwanza.  
  Hadi sasa Samatta amecheza mechi 51 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga mabao 18.
  Kati ya mechi hizo 51, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 32 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 31 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 21 msimu huu.
  Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 18, 12 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
  Vikosi vilikuwa; KV Kortrijk : Kaminski, Goutas, De Smet (74 'Ouali), Saadi (64' Kage), Van der Bruggen, Barbaric, Mercier (56 'Chevalier), Rolland, Totovitskyi, D'Haene, Van Loo
  KRC Genk : Ryan, Nastic, Walsh, Dewaest, Boëtius (60 Trossard) Naranjo, Colley, Malinovskyi (74 'Kumordzi), Buffalo, Writers, Heynen
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA APUMZISHWA GENK IKISHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top