• HABARI MPYA

  Wednesday, April 19, 2017

  RONALDO APIGA HAT TRICK, REAL MADRID YATOKA NYUMA NA KUITUPA NJE BAYERN

  Cristiano Ronaldo akiwa ameshika mpira kwa furaha baada ya kukabidhiwa kufuatia kuifungia Real Madrid mabao matatu katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Bayern Munich usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu kwenye mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo kutinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-2, baada ya wiki iliyopita kushinda 2-1 Uwanja wa Allianz Arena.
  Dakika 90 zilimalizika Bayern wakifanikiwa kulipa kisasi cha kipigo cha 2-1 baada ya mabao ya Robert Lewandowski dakika ya 53 kwa penalti na Sergio Ramos aliyejifunga dakika ya 77 huku la wenyeji likifungwa na Ronaldo dakika ya 76.
  Mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza ambako Real waliongeza mabao matatu, mawili akifunga Ronaldo dakika ya 104 na 109 na lingine Marco Asensio dakika ya 112 na kufanikiwa kuwapa nje Bayern wakiingia Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa mara ya saba mfululizo ambayo ni rekodi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO APIGA HAT TRICK, REAL MADRID YATOKA NYUMA NA KUITUPA NJE BAYERN Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top