• HABARI MPYA

  Saturday, April 15, 2017

  OMOG AWAANZISHA PAMOJA BLAGNON NA MAVUGO LEO SIMBA NA TOTO

  Na Steven Kinabo, MWANZA
  KOCHA wa Simba, Mcameroon Joseph Marius Omog leo amemuanzisha mshambuliaji Frederick Blagnon kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  Blagnon anaanzishwa leo baada ya Jumatatu kutokea benchi na kufunga mabao mawili, Simba ikitoka nyuma kwa 2-0 na kushinda 3-2 dhidi ya Mbao FC hapo hapo Kirumba na leo atacheza na Mrundi Laudit Mavugo.
  Laudit Mavugo na Frederick Blagnon wameanzishwa pamoja leo Simba dhidi ya Toto

  Kwa ujumla, kikosi cha Simba SC leo kipo hivi; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Juuko Murshid, James Kotei, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Frederick Blagnon, Laudit Mavugo na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim.
  Katika benchi wapo Peter Manyika, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamad Juma, Pastory Athanas, Ibrahim Hajib na Juma Luizo.
  Toto nao wameshatoa kikosi chao na kipoa hivi; Mwasa Mohammed Kirungi, Juvenary Pasrory Joseph, Ramadhani Adam Malima, Hamim Abdul Karim,Yussuf Suleiman Mlipili,Carlos Protas Kirenge, Jamal Soud Mtengeta, Hussein Suleiman Kasanga,Waziri Junior Shentembo, Reliant Lusajo Mwakasagule na Jaffar Mohammed. 
  Katika benchi wapo Mohammed Aziz, Mhando Robert Washa, Ladislaus Mbogo, Msafiri Ali Khamis, Mohammed Athumani Soud, Hamad Nathaniel Mbumba na Waziri Ramadhani Hussein.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OMOG AWAANZISHA PAMOJA BLAGNON NA MAVUGO LEO SIMBA NA TOTO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top