• HABARI MPYA

    Sunday, September 18, 2016

    WAZIRI NAPE AWAJAZA MANOTI WACHEZAJI SERENGETI BOYS, AWAAHIDI ZAIDI WAKISHINDA LEO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo amewakabidhi Sh. 200,000 kila mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania, Serengeti Boys kabla ya mchezo wao na Kongo - Brazaville.
    Serengeti Boys watamenyana na Kongo Brazaville saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za vijana Afrika mwakani Madagascar. 
    Na mapema leo, Nnauye ametoa Sh 200,000 kwa kila mchezaji zilizotokana na kundi michango ya kikundi cha waandishi wa habari wa michezo, waliochangisha Sh 2,600,000 wakati nyingine zilitoka kwa wadau wengine.

    Na Nape ameahidi pia kununua bao moja kwa Sh 500,000 na atalipa fedha hizo kadiri ya idadi ya mabao hata kama yatafika 10 hivyo gharama yake itakuwa Sh 5,000,000. “Kuna wabunge na viongozi wengine wameahidi kutoa fedha zaidi, kwa hiyo Serengeti Boys kazi kwenu kutafuta ushindi leo mbele ya Watanzania watakaoingia uwanjani bure.”
    Nape pia ametangaza kwamba Serikali imemua wananchi waingie bure leo kwenye mechi hiyo.
    Serengeti itahitaji ushindi mzuri leo ili kulainisha mazingira kwenye mchezo wa marudiano Oktoba 2, mwaka huu mjini Brazzaville.
    Mechi hiyo itachezeshwa na marefa kutoka Shelisheli , Nelson Fred atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na Hensley Petrousse na Stive Marie washika vibendera, mwamuzi wa akiba Allister Barra na Kamisaa Gladmore Muzambi kutoka Zimbabwe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI NAPE AWAJAZA MANOTI WACHEZAJI SERENGETI BOYS, AWAAHIDI ZAIDI WAKISHINDA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top