• HABARI MPYA

  Monday, September 12, 2016

  MCHEZAJI WA BURKINA FASO AFIA UWANJANI UFARANSA

  MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Burkina Faso, Ben Idrissa Derme amefariki dunia akiichezea mechi ya Kombe la Ufaransa klabu ya ridhaa, AJ Biguglia.
  Mwanasoka huyo aliyekuwa ana umri wa miaka 34 akipatwa shinikizo la damu mapema kipindi cha pili katika mchezo huo wa Raundi ya Tatu akiichezea timu ya Daraja la Sita Ufaransa.
  Ben Idrissa Derme amefariki dunia akiichezea mechi ya Kombe la Ufaransa klabu ya ridhaa, AJ Biguglia

  Pamoja na kupatiwa huduma ya kwanza uwanjani, lakini timu ya matabibu haikuweza kuokoa maisha yake.
  Derme amewahi kuichezea mechi nne Burkina Faso na amecheza timu za madaraja ya chini Ufaransa na Moldova sambamba na Burkina Faso.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI WA BURKINA FASO AFIA UWANJANI UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top