• HABARI MPYA

  Monday, September 12, 2016

  KILI QUEENS YAWAFUMUA 3-2 RWANDA NA KUTINGA NUSU FAINALI YA CHALLENGE JINJA

  Na Mwandishi Wetu, JINJA
  TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imefuzu Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Rwanda leo Jinja, Uganda.
  Kwa kuwa Kundi B lina timu tatu, nyinginr Ethiopia – ushindi wa leo unaihakikishia Kili Queens tiketi ya Nusu Fainali.   
  Mabao ya Kili Queens inayofundishwa na Sebastian Nkoma, yamefungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ dakika za 11 na 65 na Stumai Abdallah dakika ya 28, wakati ya Rwanda yamefungwa na Ibangarrue Marie na Amina Ally wa Tanzania Bara aliyejifunga.
  Kikosi cha Kilimanjaro Queens kilichoshinda 3-2 dhidi ya Rwanda leo mjini Jinja, Uganda

  Kili Queens watashuka tena dimbani kumenyana na Ethiopia Septemba 16, mwaka huu katika mchezo wa mwisho wa kundi lake. Rwanda na Ethiopia zitakamilisha mechi za Kundi B kwa kumenyanaa na Septemba 14.
  Nusu Fainali zitafuatia Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba 20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
  Mchezaji wa Kili Queens akifumua shuti leo Jinja dhidi ya Rwanda
  Mchezaji wa Kili Queens akimiliki mpira mbele ya wacheaji wa Rwanda leo Jinja


  Manahodha wa Tanzania Bara (kushoto) Sofia Mwasikili na wa Rwanda (kulia)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILI QUEENS YAWAFUMUA 3-2 RWANDA NA KUTINGA NUSU FAINALI YA CHALLENGE JINJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top