• HABARI MPYA

  Sunday, September 18, 2016

  MAZEMBE YATANGULIZA KIFUA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  TOUT Puissant Mazembe ya DRC imebisha hodi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya wenyeji, Etoile du Sahel Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia usiku wa jana. 
  Wenyeji walitangulia kwa bao la kiungo Hamza Lahmar dakika ya 20, kabla ya Rogger Assale kuisawazishia Mazembe dakika ya 52.
  Mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu aliyekuwa majeruhi ameendelea kuwa nje baada ya kuanza mazoezi mepesi wiki mbili zilizopita.
  Mazembe sasa watahitaji hata sare ya 0-0 katika mchezo wa marudiano nyumbani Septemba 25 mjini Lubumbashi ili kwenda fainali, ambako watakutana na mshindi kati ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria na FUS Rabat ya Morocco zinazomenyana leo Uwanja wa Unite Maghrebine katika mchezo wa kwanza pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YATANGULIZA KIFUA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top