• HABARI MPYA

  Sunday, September 11, 2016

  MAVUGO, HAJIB WAENDELEA KUING’ARISHA SIMBA SC LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifikia kwa pointi Azam FC kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hao, Ibrahim Hajib na Laudit Mavugo yote kipindi cha pili na sasa Simba SC inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne, wakishinda tatu na sare moja. 
  Laudit Mavugo akishangilia baada ya kufunga bao la pili la Simba leo
  Hajib alifunga dakika ya 52 kwa kichwa akimalizia kona nzuri iliyochongwa na beki Mohammed Hussein 'Tshabalala', wakati Mavugo alifunga dakika ya 66 akiwa ndani ya boksi baada ya pasi ya kiungo Mwinyi Kazimoto.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Frederick Blagnon dk61, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib/Jamal Mnyate dk75 na Mwinyi Kazimoto/Said Ndemla dk70.
  Mtibwa Sugar; Abdallah Makangana, Ally Shomary, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Kevin Friday/Mohammed Juma dk57, Ally Yussuf, Stahmili Mbonde, Ibrahim Juma/Hussein Javu dk73 na Haroun Chanongo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAVUGO, HAJIB WAENDELEA KUING’ARISHA SIMBA SC LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top