• HABARI MPYA

  Monday, May 09, 2016

  WACHEZAJI SIMBA SC WAGOMA KWENDA SONGEA KISA; “KAZI BILA MUSHAHARA”

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI saba wa Simba wakiwemo sita wa kigeni, wamegoma kusafiri kwenda Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Majimaji Jumatano.
  Simba inatarajiwa kumenyana na Majimaji keshokutwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea katika hatua ya lala salama ya Ligi Kuu.
  Na nyota sita wa kigeni, kipa Vincent Angban (Ivory Coast), mabeki Emery Nimubona (Burundi), Juuko Murshid (Uganda), viungo Justice Majabvi (Zimbabwe), Brian Majwega (Uganda), Hamisi Kiiza (Uganda) wamegoma kusafiri.
  Hamisi Kiiza ni miongoni mwa wachezaji waliogoma kwenda Songea na kikosi cha Simba

  Kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto ni mchezaji pekee anayetumia hati ya kusafiria ya nyumbani aliyegoma kusafiri na wote ni kwa sababu moja, wamecheleweshewa mishahara ya Aprili.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba sababu ya kuchelewa kuwapa mishahara wachezaji wao inatokana na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuchelewa pia kuwapatia fedha za udhamini.
  Pamoja na waliogoma, Manara amesema Raphael Kiongera, Jonas Mkude, Awadhi Juma na Ibrahim Hajib nao hawajasafiri na timu kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuwa majeruhi na kutumikia adhabu za kadi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WACHEZAJI SIMBA SC WAGOMA KWENDA SONGEA KISA; “KAZI BILA MUSHAHARA” Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top