• HABARI MPYA

    Tuesday, May 10, 2016

    ULIMWENGU: PENGO LA SAMATTA SASA LINANEKANA MAZEMBE

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Thomas Emmanuel Ulimwengu amesema kwamba kwa sasa pengo la Mtanzania mwenzake, Mbwana Ally Samatta linaonekana TP Mazembe.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE  jana, Ulimwengu alisema Mazembe kwa sasa inamkosa mjanja  na mwepesi, mwenye uwezo wa kufunga kama Samatta.
    Samatta aliondoka timu hiyo ya DRC Januari mwaka huu baada ya kushinda nayo taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na kujiunga na KRC Genk ya Ubelgiji anakoendelea vizuri hivi sasa.
    Na tangu kuondoka kwa Samatta aliyekuwa kinara wa mabao wa timu hiyo ya Lubumbashi, Mazembe imeonekana kupoteza makali yake kiasi cha kuvuliwa mapema ubingwa wa Afrika.
    Thomas Ulimwengu (kulia) akiwa na Mbwana Samatta (kushoto) walkipokutana tena kwa majukumu ya kimataifa baada ya kuachana Lubumbashi 

    Mazembe ilitolewa na Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na kuangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. Lakini juzi, Mazembe ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Stade Gabesien Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
    Na baada ya matokeo hayo, Ulimwengu aliyecheza kwa dakika 45 juzi kabla ya kutoka uwanjani anachechemea, amesema timu kwa sasa haina mtaalamu wa kufunga mabao kama alivyokuwa Samatta.
    “Pengo la Samatta linaanza kuonekana sasa, pale mbele hakuna na anayeweza kufunga kama Samatta, tunapoteza nafasi nyingi sana, hilo ndilo tatizo,”amesema Ulimwengu.
    Sasa Mazembe itakuwa na kibarua kigumu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ikitakiwa kwenda kuulinda ushindi huo mwembaba nchini Tunisia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ULIMWENGU: PENGO LA SAMATTA SASA LINANEKANA MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top